October 21, 2014

BENKI YA PIOSTA TANZANIA YATAKA WANAFUNZI KUWA NA UTAMADUNI WA KUWEKA AKIBA ILI IWASAIDIE BAADAE

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TBP), Sabasaba Moshingi akitoa Elimu ya Kifedha kuhusu umuhimu wa kufungua Akaunti kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Kujiwekea Akiba Duniani.
 Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TBP), Sabasaba Moshingi.
 Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Nora Daniel akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi.
 Diana Daniel akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani. Wa pili kushoto ni Nora Daniel na Diana Daniel mara baada ya kukabidhiwa zawadi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani. Wa pili kushoto ni Nora Daniel na Diana Daniel mara baada ya kukabidhiwa zawadi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kufugua akaunti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mauzo wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Nelson Mwakilasa (katikati) akiwaonyesha kadi ya kutolea fedha katika mashine baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam wakati uongozi wa benki hiyo ulipofika shuleni hapo na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kufungua akaunti kwa wanafunzi hao. 

Na Mwandishi Wetu

UONGOZI wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) umewataka wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kujiwekea akiba itakayowasaidia katika maisha yao wakati wowote.

Akizungumza na wanafunzi sambamba na walimu wa shule ya Sekondari Jangwani Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi alisema asilimia 14 tu ya wananchi ndio wanaoweka akiba jambo ambalo alisema kuwa ni idadi ndogo.

Alisema ni muhimu kwa kila mtanzania kuweka akiba na ikiwa mwezi huu ni tarehe 30 Duniani ni siku ya kuweka akiba ambayo benki ya Posta ni mwanachama.

“Idadi ni ndogo sana ya watu kujiwekea akiba kwa kuwa hadi sasa asilimia 14 tu ya watanzania ndio wanaweka mikopo benki na asilimia 3% ndio wanaochukua mikopo hivyo ni vyema kuitumia siku hii kwa kuwataka watanzania kuweka akiba na kuchukua mikopo kwa maendeleo yao,”alisema Moshingi.

Alisema benki ya Posta itakuwa katika matembezi kwa kuwafuata wateja wao na kwamba wameona umuhimu wa kuwatembelea wanafunzi wa Jangwani hasa kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.

Alisema amekuwa akisikitishwa sana na kitendo cha watoto wakike kutopata elimu hasa wa Serengeti anapotoka yeye hivyo amewataka pia wazazi kuwawekea akiba watoto hasa katika benki hiyo.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Geraldin Mwanisenga alisema  shule ya Jangwani ina wanafunzi 1100 licha ya kuendelea na usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza na tano.

Aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kufika shuleni hapo na kutoa elimu kwa wanafunzi hao huku akiwataka kuendelea kufanya hivyo mara kwa mara.

Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja Grace Nkuzi aliwaeleza wanafunzi hao kuwa TPB ina akaunti mbalimbali ambazo zitamfanya mwanafunzi aweze kusoma akiwa na akiba yake itakayomuendeleza hapo baadaye.

Alisema kuna akaunti ya Platinum haina makato na unatumia kadi ya ATM kwa zaidi ya mabenki 20,000 na kwamba inatumia Umoja Switch.

Naye Afisa Mahusinao Joyce Magige aliwataka wanafunzi hao kuweka akiba kwa kuwa ni kitu muhimu kwao kwa maisha ya sasa na baadaye.

No comments:

Post a Comment

Pages