Meneja wa Benki ya Exim wa Tawi Moshi mkoani
Kilimanjaro, Bw. John Ngowi akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti
lililofanyika baada ya benki hiyo kutembelea kituo cha Wazee cha Njoro katika
manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Mbali na kupanda miti, benki pia ilitoa
msaada wa chakula katika kituo hicho. Wakishuhudia ni wafanyakazi wa Benki ya
Exim jijini Moshi.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Moshi, Kilimanjaro wakimshuhudia mmoja kati ya wanajamii wa Njoro akishiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanywa na Benki hiyo baada ya kutembelea kituo cha Wazee cha Njoro katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Mbali na kupanda miti, benki pia ilitoa msaada wa chakula katika kituo hicho.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Moshi, Kilimanjaro wakimshuhudia mmoja kati ya wanajamii wa Njoro akishiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanywa na Benki hiyo baada ya kutembelea kituo cha Wazee cha Njoro katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Mbali na kupanda miti, benki pia ilitoa msaada wa chakula katika kituo hicho.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Moshi,
Kilimanjaro wakimshuhudia mmoja kati ya wanajamii wa Njoro akishiriki katika zoezi
la upandaji miti lililofanywa na Benki hiyo baada ya kutembelea kituo cha Wazee
cha Njoro katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Mbali na kupanda miti,
benki pia ilitoa msaada wa chakula katika kituo hicho.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Benki ya Exim Tanzania imepanda miti mia moja kuzunguka eneo la kituo
cha wazee wasiojiweza cha Njoro jijini Moshi, hatua iliyofikiwa kutokana na jitihada
za Benki hiyo za uboreshaji mazingira kupitia mpango ujulikanao kama ‘go-green’
ambao umelenga kuziunga mkono jitihada za serikali nchi nzima katika utunzaji
wa mazingira.
Benki pia katika tukio hilo ilitoa msaada wa chakula katika kituo
hicho cha wazee. Mchango huo ukiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo za
kijamii.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Meneja Mkuu wa Tawi la Benki ya Exim
Moshi, Bw. John Ngowi alisema utunzaji mazingira ni sehemu ya jitihada za Benki
katika shughuli za kijamii ambazo uendana na mpango wa benki wa ‘Go – Green’
ambao umelenga kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kulinda uhalibifu
wa mazingira.
Alisema kuwa miti hiyo mia moja iliyopandwa ikitunzwa vizuri
itawawezesha wazee katika kituo hicho kuwa na mazingira mazuri na hali ya hewa
safi. Aliongeza kuwa mbali na zoezi hilo la upandaji miti, Benki pia imechangia
chakula katika kituo ili kuwasaidia wazee katika mahitaji yao muhimu, hatua
ambayo ni sehemu ya shughuli za kijamii ya benki hiyo.
“Katika Benki ya Exim
tunazitazama shughuli za kijamii kama uwekezaji katika jamii, ambao utiliwa
mkazo na kanuni ya ‘Kurudisha Kile Tulichonacho kwa Jamii’. Jitihada katika
shughuli za Benki za kijamii zimejikita katika maeneo makuu manne ambayo ni:
Mazingira; Elimu; Afya; na Maendeleo ya Michezo,” alisema Bw. Ngowi.
Bw. Ngowi alisema kuwa dhamira za benki haijikiti pekee katika
kuongeza mizania ya benki lakini pia kuhakikisha inarudisha kile ikipatacho kwa
jamii ambayo inaizunguka.
“Kupitia mwendelezo wa jitihada zilizoonyeshwa na wafanyakazi wa Benki
ya Exim na menejimenti yake, tunaamini kuwa benki yetu itatoa mchango mkubwa
katika maendeleo ya jamii nchi nzima.
“Natumai mchango wetu katika
kituo hichi cha wazee utakuwa na manufaa makubwa baadae. Uzoefu huu hautukumbushi
tu kuwa ni muhimu kutoa kile tulichonacho kwa jamii lakini pia inatufundisha
kufanyakazi kwapamoja kama timu,” alisema.
No comments:
Post a Comment