November 01, 2014

Benki ya Posta kutoa Mkopo wa basi kwa timu ya Mbeya City FC

Na Kenneth Ngelesi, MBEYA

BANKI ya Posta nchini (TPB) imekubali kutoa mkopo wa basi lenye dhamani ya shilingi milioni 300 kwa timu ya Soka ya Mbeya City FC kwa ajili ya safari mbalimbali za kushiriki ligi kuu Tanzania.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na  Kaimu Mkurugenzi wa Bank hiyo Jema Msuya wakati wa hafla ya kuzindua akaunti maalumu kwa mashabiki na wadau timu hiyo ilifanyika katika Hotel ya GR iliopo katika eneo la Sowetho na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk Norman Sigalla aliye mwakilisha Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Hata hivyo Msuya alikfikia hatua ya kutoa ahadi kutoa ahadi hiyo ambayo utukelezaji wake utaanza hivi punde baada ya Meya wa jiji la Mbeya Athanus Kupunga kuiomba benki kutoa mkopo wa basi ili kuepusha upotevu wa fedha zinatumika kwa ajili ya kukodi basi la wachezaji.

Akizungumza kataika hafala hiyo Meya Kapungu alisema sema kuwa kutoka na mashabiki pamoja na timu kwa ujumla kutumia magari ya kukodi na ambaye kimsingi gharama yake ni kubwa hivyo ni vema banki hiyo ikatoa Mkopo huo ili fedha zinazotumika kukodisha basi hilo zitumike kwa ajili ya kulipia deli hilo.

‘Kwanza niwapongeze ndugu zangu wa Banki posta kwa kumua kutoa huduma hii ya ambayo kimsingi itasaidia sana wadau na mashabiki kuichangia timu yetu lakini ni hili niwatoe hofu mfika maalai sahihi na hamajapotea,pia niwaombe mtu sadidie kutukopesha basi kwa ajili ya wachezaji na mashabiki ili fedha tunazo tumia kukodi zitumike kulipia deni’ alisema Kapunga.
Katika hatua nyingine Meya Kapunga aliwataka wadau na wapenzi wa timu hiyo kuwa na moya wa subra katika kipindi hiki cha mpito ambacho timu hiyo imekuwa na matokeo mabaya kwa mechi tatu mfurulizo.

Kapunga alisema kuwa kuelekea mchezo wa Jumapili dhidi ya Mgambo Shoting, amepanga kukutana na mmoja mmoja ili kubaini matatizo yao kwani wakiuzwa  kwa pamoja wamekuwa wagumu kueleza yanayo wasibu.

‘Napenda niwa hakikishie ndugu zangu ninakwenda Tanga na nitakukutana na mchezji mmoja mmoja ili kupata dukuduka zao kwani huenda mwingine anauguliwa na mke wake ama mzazi wake na matatizo mengine, hivyo kueleza mbele ya kundi ni vigumu’ aliongeza Kapunga.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kutoka Mkoa wa Mbeya kutambua kuwa timu hiyo ndiyo iliyobeba sura ya Mkoa hivyo wanapaswa kuiunga Mkono kwa kufungua akaunti ya kuchangia katika Benki ya Posta na kwamba timu hiyo ni mali  ya Serikali ambapo Serikali yenyewe ni wananchi.

Kwa upande wake kabla ya kutoa ahadi ya kutoa Mkopo wa basi hilo Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo Msuya aliwataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kujiunga huduma hiyo kwani mbali na kuchangia timu yao kwa njia ya kukatwa shilingi 200 kila mwezi lakini kwa ajili ya kuichangia timu yake wakati huo huo akaunti hiyo itamuwezesha mshabiki kupata huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo fursa ya kupata Mkopo.
 Mbali na huduma ya Mikopo lakini pia shabiki akiwa na kadi hiyo ataweza kupata huduma ka kutoia fedha kupitria mashine yeyte ya ATM huku namaba ya simu ikiwa imeunganishwa na huduma ya kibenki.
Naye mgeni Rasmi mkatika hafla hiyo  DK Sigalla akizungumza na mimia ya mashabiki wa timu ya Mbeya City alipongeza kitendo cha uvumilivu ikilichonyeshwa mashabiki na mashabiki wa katika kipindi hiki ambapo timu imekuwa ikifanya vibaya mfurulizo na kwamba kipindi hicho ni cha mpito hivyo ambako kila timu zimekuwa zikipitia.
Aidha katika hatua nyingine Dk Sigalla mara baada ya kutoa hutuba hiyo alikadhiwa kadfi yake huku akiwatoa wito kwa viongozi kuanzia Meya,Mkurugenzi wa jiji , Kaimu wake,Mwenyekiti wa timu, na viongozi wengine kaunza kukatwa shilingi 200,000/ kila mwezi badala ya shilingi 200 ili kutunisha akaunti timu kwa haraza zaidi.
Katika hafla hiyo ambayo ilihudhiriwa na watumishi mbalimbali wa Benki hiyo kutoka Mkoa wa Mbeya,Uongozi wa timu ya Mbeya City pamoja na wapenzi na mashabiki, zaidi ya shilingi million I moja zilichangawa kwa ajili ya nauli ya mashabiki watao enda kuishangalia timu hiyo siku ya jumapili jiji Tanga utakapo kuwa ikumana na Mgambo Shoting katika uwanja wa Mkwakwani huku Benki ya posta ikitoa shilingi laki tano.

No comments:

Post a Comment

Pages