November 07, 2014

MSHINDI WA TMT 2014 MWANAAFA MWINZAGU AFAULU MITIHANI YAKE YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2014.

 Pichani (Katikati) ni Mwanaafa Mwinzagu ambae ni Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wafanyakazi na Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya kutangazwa mshindi wa Kitita cha Milioni 50 za Kitanzania katika fainali ya shindano la TMT lililomalizika Mnamo tarehe 30 Aug 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City na Kumtangaza Mwanaafa Kuwa Mshindi kwa Mwaka 2014.

Na Josephat Lukaza 

Mwanaafa Mwinzagu ambae alishiriki Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) huku akiwa ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Tandika iliyopo Mjini Mtwara katika Manispaa ya Mtwara amefaulu mitihani yake ya kumaliza elimu ya Msingi Kwa Kupata daraja C huku Masomo ya Hesabu na Sayansi akiwa kafanya vizuri sana kwa Kupata Daraja B.

 Wakati Shindano la TMT lilipofika Mtwara kwaajili ya kusaka vipaji vya kuigiza Ndipo Mwanaafa alipojiunga na Kuja kushiriki Katika SHindano hilo Kubwa na lenye mvuto wa Pekee Afrika Mashariki na Kati. Wakati akihojiwa mara baada ya Kutoka katika hatua ya Kwanza ya Shindano hilo lililofanyika Mtwara na kuhojiwa Mwanaafa Mwinzago alisema "Hiki ni Kipaji kwahiyo sina haja ya kuficha na pia naweza Kukosa kwenye Shule nikapata Kwenye Kuigiza na ndio maana nimekuja Kushiriki" Vilevile alipoulizwa Je Ikitokea Ukashinda itakuwaje Shule na Sanaa? Alijibu kuwa "Ikitokea nikashinda katika ngazi ya Kanda ya Kusini Nitaenda Kambini Dar Es Salaam na kuacha Shule kwanza, Maana Shule Ipo ila Shindano hili linapita tu Kwahiyo Naweza kupata kwenye Sanaa na nikishinda basi nitarudia Darasa". BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»

Mara baada ya Kuibuka MShindi katika Kinyanganyiro Hiko Katika Ngazi ya Kanda ya Kusini, Timu nzima ya TMT iliweza kumuhoji Mwalimu wake Mkuu ambapo alisema yafuatayo "Huyu Ni mwanafunzi wa Darasa la Saba Kwa Sahivi na Hiki pia ni kipaji lakini Sisi kama Wazazi hatuwezi kuzuia Mtoto kuonyesha Kipaji chake yeye alichofanya alishiriki Mashindano na ameshinda kwahiyo sisi kama walimu wake tutajadiliana jinsi ya kulitatua hili kwa maana hatuwezi kujua labda mshindi wa Milioni 50 hatakuwa yeye"

Mara baada ya Shindano la TMT kumalizika tarehe 30 August 2014 wiki moja baadae Mwanaafa aliweza Kurejea Mjini Mtwara kwaajili ya Kufanya mitihani yake ya Kuhitimu Elimu ya Msingi na Hatimae mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Mwanaafa aliweza kwenda shule kwao kwaajili ya kukamilisha taratibu za kufanya mtihani na kesho Mwanaafa akaweza kufanya Mitihani yake vizuri kwa muda wa siku mbili na alipomaliza Alirejea Jijini Dar Es Salaam ambapo Aliendelea na zoezi la Kurekodi filamu ya Pamoja Ya Washindi wa TMT waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi Bora huku yeye akiwa ni kinara katika filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Mapema Mwezi wa Kumi na Mbili katika Mikoa yote ambayo TMT ilipita kwaajili ya kusaka Vipaji.

Hapo Majuzi kupitia Vyombo mbalimbali vya habari kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya Mitihani ya Elimu ya Msingi na Ndipo tulipofahamu kuwa Mwanaafa ameweza kujitahidi sana katika Mitihani huku akiwa kafanya Vizuri sana katika Masomo ya Hesabu na Sayansi ambapo amepata daraja B huku masomo mengine akiwa amepata daraja C na Kupelekea kupata wastani wa daraja C.

Kwa Matokeo hayo tunapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kuonyesha uwezo wake katika Masomo na hatimaye kufanya vizuri katika Mitihani yake ya Mwisho ya Kumaliza Elimu ya Msingi
Ikumbukwe kuwa hapo awali Mwanaafa alisema kuwa endapo atashinda Milioni 50 katika fainali ya Shindano la TMT lililomalizika tarehe 30 August 2014 basi atatumia Kiasi hiko cha pesa kwaajili ya kujiendelea kielimu lakini Wakati wa Fainali hiyo Kampuni ya Proin Promotions Ltd iliahidi kumsomesha Mwanaafa hata Kama asingeshinda katika Shindano hilo.

Kwasasa Mwanaafa yupo chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions ambapo kampuni hiyo itamsomesha Kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Cha Nne.

Kampuni ya Proin Promotions Ltd inapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kufanya Vizuri katika Mitihani yake ya Kumaliza Elimu ya Msingi na kuonyesha Kuwa Kumbe Bado ni Mshindi hadi Darasani.

No comments:

Post a Comment

Pages