November 12, 2014

OPARESHENI DELETE CCM YAINGIA KIGOMA

Waliokuwa viongozi wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga kupitia CCM, wakionyesha kadi zao kabla ya kuzikabidhi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipojiunga na chama hicho wakati wa mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijiji hapo juzi. (Picha zote na Joseph Senga)
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM.
Akinamama wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakicheza ngoma ya asili, wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), baada ya kuwasili kijijini hapo, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM.
 Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Taifa la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Julius Mwita (kushoto), akimkabidhi kadi ya chama hicho, Mwenyekiti wa Kijiji cha Udomo Kata ya Uchama Jimbo na Wilaya ya Bukene mkoani Tabora, Julius Lubala, baada ya kurudisha kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment

Pages