November 01, 2014

WAZIRI WA AFYA SEIF RASHIDI AZINDUA RASMI GHETTO RADIO KATIKA HOSIPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR

Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid akiongea na Wauguzi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke, Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio hiyo, ambayo lengo lake ni kuwakomboa vijana wa Mtaani pamoja na vipindi vingine vya kuelimisha Jamii na Burudani, Pia amewashukuru kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo vitasaidia katika Hospitali hiyo leo Tarehe 1.11.2014
 Mkurugenzi wa Sibuka George Ndagali akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm iliyo fanyika katika  katika Hosipitali Teule ya Mkoa wa Temeke Ambapo Ghetto Radio Imeweza kufunguliwa Rasmi Katika Mkoa huo nakuweza kutoa Msaada Vifaa Mbalimbali pamoja na Madawa Ambavyo Vyote kwa ujumla vimegharimu kiasi Cha Shilingi Milioni sita na Laki sita.
 Mkurugenzi wa Ghetto Radio Matt Brouwer akizungumza neno wakati wa uzinduzi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Ambapo Bw.Brouwer Alisema kuwa Ghetto Radio ilianzishwa nchini Kenya Miaka Sita iliyopita nakuweza kuwasaidia vijana mbalimbali Hivyo wameweza kuingia Nchini Tanzania Ilikuendeleza kuwapa vijana Fursa Na elimu INayo Tolewa na Kituo Hicho Kwa Hapa Nchini
Mganga Mkuu wa Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke Amaani K. Malima akitoa neno la Shukurani kwa Timu nzima ya Ghetto Radio ya Sibuka Fm kwa kufanya uzinduzi wa Radio yao katika Hospitali hiyo pia kutoa Msaada wa vitu mbalimbali vitakavyo saidia katika eneo hilo.
 Meneja wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm  Edward  Lukaka  akitoa maelezo machache ya malengo ya Radio hiyo pia kueleza mikakati ya kuendelea kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba katika Vituo zaidi vya Afya.
 Mkurugenzi wa kituo cha afya cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi akiwashukuru Ghetto Radio ya Sibuka FM kwa kuanzisha Kituo hicho pia na wao wametoa vifaa vya matibabu kwa ajili ya kushiriki uzinduzi huo wa Radio
 Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Dar es salaam Leonard Masonu  akitoa neno la Shukurani
Hivi ni Baadhi ya vitu ambavyo vimetolewa na Ghetto Radio ya Sibuka Fm katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio hiyo
 Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid akikabidhiwa Rasmi msaada wa Vifaa na Vitu mbalimbali vitakavyo tumika katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke kutoka kwa Ghetto Radio ya Sibuka Fm

Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid kushoto  Akishukuru kwa vifaa hivyo.

 Baadhi ya Wadau mbalimbali walioshiriki katika Sherehe hiyo ya Uzinduzi Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
 Baadhi ya Wauguzi wakiwa katika uzinduzi huo Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
 Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakijiandaa kuelekea kutoa Msaada wa vitu mbalimbali katika vyumba vya wagonjwa
  Wakiwa wanaelekea Wodini
 Kulia ni Mkurugenzi wa Sibuka George Ndagali akiwa katika Wodi ya watoto kukabidhi zawadi za watoto na mama zao, katikati ni Mwanamuziki Mkongwe wa Bongo Flava Juma Nature ambaye ni Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm


Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Juma Nature akiwa anatandika Shuka moja wapo katika Wodi ya watoto kuashiria kukabidhi mashuka hayo.
Baadhi ya Timu ya wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm


No comments:

Post a Comment

Pages