Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MB Mobile ya Maendeleo Benki uliofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (wa tatu kushoto) akizindua huduma mpya ya MB Mobile ya Maendeleo Benki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Banki, Ibrahim Mwangalaba, Mkurugenzi wa Benki hiyo, Balozi, Richard Mariki na Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dk. Alex Malasusu.
Tunazindua...............???
Tumezindua.......huduma mpya.
Huduma mpya ya MB Mobile yazinduliwa.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa mara baada ya kuzindua huduma mpya ya MB Mobile
Mmeona zawadi niliyopewa...................????
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (katikati) akiteta jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa mara baada ya kuzindua huduma mpya ya MB Mobile.
Picha ya pamoja ya wakaurugenzi.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Maendeleo Bank
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (katikati) akibadilishana mawaz na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa (kulia) mara baada ya kuzindua huduma mpya ya MB Mobile
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amewataka
Watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam katika uzinduzi
wa huduma mpya ya 'MB mobile'
ulioanzishwa na Benki ya Maendeleo.
Alisema ili Nchi yoyote duniani ipige hatua uwekaji wa
akiba ni jambo muhimu sana, hivyo Watanzania wanapaswa kujenga utamaduni huo
ili kwani ndio njia pekee ya kujipatia maendeleo kwa urahisi.
Mwigulu alisema hiyo ni hatua mojawapo ya maendeleo
ambayo benki hiyo imepiga kwani hivi sasa wateja wao hawatapata shida ya
kuhangaika kuweka au kutoa fedha.
"Benki ya Mkombozi haina muda mrefu lakini
inaonekana inapiga hatua kubwa kimaendeleo, hivyo nawaomba Watanzania wasiwe na
hofu kuweka akiba katika benki hii kwani fedha zao zitakuwa sehemu
salama," alisema Nchemba.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ibrahim
Mwangalaba, alisema benki yao ina mwaka mmoja na miezi mitatu tangu ianzishwe
lakini wanashukuru wanakwenda vizuri.
Alisema hadi sasa ina wateja 7,000 na wameweza kukusanya
amana zaidi ya sh. bilioni 15.5 na pia imechangia kuongeza kasi ya ukuaji
uchumi nchini kwa kutoa mikopo ya zaidi ya sh. bilioni 10.
Aliongeza kuwa kupitia huduma hiyo mpya ya MB Mobile
wateja wataweza kutumia huduma ya kifedha bila kujali eneo, kwa kuangalia
salio, kuweka pesa kwenye akaunti zao kwa kupitia Tigo pesa na M-Pesa.
No comments:
Post a Comment