January 21, 2015

MBUNGE FILIKUNJOMBE ATOA MSAADA WA ZAIDI YA TSH MILIONI 15 UKARABATI WA KANISA LA RC MADUNDA

Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akizungumza na  waumini wa kanisa la RC Madunda mara  baada ya  kusaidia kanisa  hilo kiasi cha Tsh milioni 15  za ukarabati wa kanisa na vinanda  viwili  vya kwaya kanisani  hapo
Viongozi  wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge  huyo kwa  msaada wake.
Waumini  wa kanisa   hilo  wakifurahia  misaada  ya mbunge  wao
katibu  mwenyezi  wa  wilaya ya  Ludewa Filix Haule  (kushoto ) na mmoja kati ya madereva wa mbunge  Filikunjombe Bw Andondile  wakisogeza  vinanda viwili vya kisasa  kwa mbunge Filikunjombe
Mbunge  Filikunjombe kulia akikabidhi  msaada wa vinanda kwa viongozi wa kwaya  katika  kanisa la RC Madunda
kiongozi  wa  kwaya kanisani hapo akifurahia  msaada wa vinanda  kulia na mbunge Filikunjombe
Mbunge  Deo Filikunjombe (kushoto) akikabidhi msaada  wa  kinanda  kwa viongozi  wa kwaya kwaya katika  kaniksa  hilo la RC Madunda  leo
Mbunge Filikunjombe kulia akizungumza jambo na  paroko msaidizi  wa Madunda  baada  ya  kutoa mchango wake wa Tsh milioni 15  kwa ajili ya  kukarabati kanisa  mchango ambae kiusalama aliahidi  kuuweka katika akaunti ya  jimbo
Mzee Nkwera  ambae ni mshauri  wa  kisiasa wa  mbunge  Filikunjombe akizungumza kanisani hapo
Bw Mgaya  akimshukuru mbunge Filikunjombe
Na matukiodaimaBlog
MBUNGE wa   jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  amechangia   kiasi cha Tsh  milioni  15  kwa  ajili ya  ukarabati wa kanisa la Roman Katoriki parokia ya  Madunda  wilayani  Ludewa pamoja na  kusaidia   vinanda viwili kwa  kwaya  mbili kanisani hapo.

Akikabidhi msaada  huo   leo   mara  baada  ya  ibada  ya  jumapili  mbunge Filikunjombe alisema  kuwa amefika  kanisani  hapo baada ya kuomba  kinada na  kwaya  ya  kanisa  hilo na  hivyo  kutokana na kuwepo kwa kwaya  mbili amelazimika   kutoa msaada  wa vinanda kwa kwaya  zote  pamoja na  kusaidia kiasi hicho cha  fedha  kwa ajili ya  ukarabati  wa kanisa  hilo.

Kwani  alisema  kuwa kanisa   hilo ni mmoja kati ya makanisa  makongwe  yaliyojengwa  miaka  ya  1980 katika wilaya   hiyo ya  Ludewa na  kuwa kanisa   hilo ndilo kanisa la tatu kujengwa kwa  wilaya ya  Ludewa hivyo  linahitaji  kufanyiwa  ukarabati  mkubwa  ili  kuendelea  kuwafanya  waumini  wa kanisa   hilo  kupata  eneo la kuabudia.

Filikunjombe  aliwataka    waamuni hao na  waumini  wa madhehebu mengine  katika  wilaya ya  Ludewa  kuendelea  kumwombea afya njema  ili  kupata  nguvu  ya  kuwaletea maendeleo kama  ambavyo  ameendelea  kufanya katika   wilaya   hiyo  kama  njia  ya  kuwashukuru  wananchi  wake  kwa  kumwamini katika  uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa  kumchagua  kuwa  mbunge  wa  jimbo hilo la  Ludewa .

"Imani  ambayo  wenzangu  wananchi wa Ludewa  mlioionyesha  mwaka  2010 katika  uchaguzi mkuu  kwa kunichagua kuwa mbunge kamwe  sitaacha  kuwakumbuka   wananchi  wangu  wa Ludewa  kila ninapokuwa bungeni  mawazo yangu  kurejesha  ahsante  yangu kwangu na  kuona   wilaya  yetu ya  Ludewa  inaendelea   kupiga  hatua"

Pia mbunge huyo  alisema  kwa  sasa  mkakati  wake na  wa  serikali ya  Rais Dr  Jakaya  Kikwete  ni  kuona  ujenzi wa barabara  ya  lami  kutoka Njombe hadi  Ludewa  inajengwa  na tayari  wakandarasi  wa  kuanza  ujenzi  huo   wamekwisha  patikana ndani ya  miaka hii miwili bararabara    hiyo  itakuwa  imejengwa na ujenzi  wake  utafanyika kwa  awamu  tofauti.

Hata  hivyo  alisema  kuwa akiwa mbunge  wa  jimbo  hilo kamwe  hatakubali kuona   wana Ludewa   anawapelekea  maendeleo kwa upendeleo na  kuwa lazima  pande zote  ikiwemo la milimani  , mwambao wote  wananufaika na matonda  yake  kwa  kuwa na maendeleo  wote.

Kwa  upande  wake  katibu  wa itikadi  na uenezi  wa  mkoa  wa Njombe  Honoratus Mgaya  akimpongeza  mbunge    huyo kwa  kuendelea   kusukuma  mbele  maendeleo ya  jimbo  hilo ,alisema  kuwa kazi zinazofanywa  na mbunge  huyo  zimekipatia  heshima chama  cha mapinduzi (CCM) na  kuwa  utendaji mzuri  wa kazi wa mbunge  huyo ndio ambao umeitangaza wilaya ya  Ludewa.

No comments:

Post a Comment

Pages