Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akiongozana na viongozi wa hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake leo katika hospitali hiyo.
NA
MWANDISHI WETU
HOSPITALI ya Aga Khan
iliyopo jijini Dar es salaam
imesema itashirikiana na hospitali ya
Temeke iliyopo wilaya ya Temeke kwa
ajili ya kuhakikisha afya ya mama na mtoto inaboreshwa.
Hayo
yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Sophia Mjema wakati ya ziara yake hospitalini hapo
kujionea huduma zitolewazo na hospitali hiyo kwa kutumia vifaa vya
kisasa.
Mjema
alisema kupitia ushirikiano huo Temeke hospitali
itapata fursa ya kupeleka wagonjwa wake
Agha Khan hasa akina mama na watoto kufanyiwa vipimo vya afya na matibabu bure .
Aidha
alisema mbali ya huduma hizo pia watalaamu wa Agha Khan watawasaidia wa Temeke katika kuwapa mafunzo
ya namna ya kutumia vifaatiba vya kisasa
hivyo kubadilisha na ujuzi.
Katika
Ziara hiyo Mjema aliwataka watanzania kuacha kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa kuwa hivi sasa kuna hospitali zinazotoa
huduma zote ambazo ziliwalazimu watu kwenda nje kutibiwa na aliwashauri watumie
hospitali hiyo ambayo ina wataalam wa kutosha hususan kwa magonjwa
yaliyoshindikana sambamba na vifaatiba vya kisasa.
Pamoja
na mambo mengne, Mjema alitoa shukrani
za dhati kwa uongozi wa Aga Khan na kuwataka waendelee na moyo huo ili kutimiza
malengo ya milenia katika sekta ya afya.
Kwa
upande wake Dk. Jaffer Dharsee wa hospitali
ya Aga Khan alisema katika kudumisha ushirikiano itatoa mashine ya CT Scan pamoja na wataalam kwaajili ya hospitali ya
Temeke ili kuwarahisishia wakazi wa
Wilaya hiyo .
Naye Bertysheba ambaye ni mgonjawa aliyekwenda
kupata huduma ya Mionzi ya kansa
hospitalini hapoa alisifu huduma
zitolewazo na Agha Khan sambamba na kuwatoa hofu wagonjwa wa kansa kutoogopa kutibiwa kwa njia ya mionzi kwani ndiyo inayompa
ahueni na anatumia kwa mwaka wa tatu sasa.
No comments:
Post a Comment