Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU ya Coastal Union ya Tanga
imesema kuwa itahakikisha inapambana vilivyo ili kuweza kuhakikisha inachukua
pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania
Bara itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Coastal Union itangia kwenye mechi
hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao ya mzunguko wa kwanza
iliyochezwa kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City iliweza
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilipatikana kwa njia ya penati.
Akizungumza maandalizi ya kuelekea
mchezo huo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa maandalizi
ya kuelekea mechi hiyo imekamilika kwa asilimia kubwa kwa kufanya mazoezi
asubuhi na jioni.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni
kuhakikisha wanafuta machungu ya kufungwa na Yanga bao 1-0, kwenye mechi yao ya
Ligi kuu iliyochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani jambo ambalo
halikuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa soka.
Aidha amesema kutokana na kikosi
chake kuendelea kuimarika kila mchezo wanaokuwa wakicheza wana matumaini
makubwa ya kupata ushindi ambao utawawezesha kusogea kwenye nafasi za juu
kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Alisema kuwa ligi kuu msimu huu imekuwa ni ngumu sana lakini kubwa ni kujipanga
hivyo wamejipanga vizuri kwa umakini mkubwa lengo likiwa kukiwezesha
kikosi hicho kinapata matokeo mazuri.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO COASTAL UNION.
OSCAR ASSENGA-0714543839
No comments:
Post a Comment