Na Mwandishi Wetu
MSANII wa
muziki kutoka kundi la ‘Chamber Squad’, Moses Bushagama ‘Mez B’, amefariki
dunia leo asubuhi Mkoani Dodoma baada ya kusumbuliwa na Homa ya mapafu kwa
muda mrefu..
Taarifa ya
kifo cha Mez B zimethibitishwa na mama yake mzazi, na kwamba alikuwa amelazwa kwenye
Hospitali ya Mwananchi.
Hivi
karibuni Mez B aliongea katika kipindi cha E-News cha EATV, alisema anaendelea
vyema.
“Nilikuwa na
tatizo la Pneumonia tokea mwezi wa 12 nikawa nipo vizuri nilivyokuja tena
Dodoma hali ikabadilika ndo nipo hospitali nimelazwa nasumbuliwa na maumivu ya
kichwa na shingo.
Nategemea
kuruhusiwa muda wowote na sasa hivi naendelea vizuri,” alisema.
Mez B amewahi
kulazwa na kuruhusiwa mara kadhaa katika hospitali ya Dodoma na hivi karibuni
alizidiwa na kulazwa mkoani humo mpaka umauti ulivyompata.
Baadhi
ya nyimbo alizowahi kuimba Mez B ni pamoja na ‘Fikiria’, ‘Kama Vipi’, ‘Kikuku’, ‘Shemeji’ ‘Nimekubali’ pamoja na ‘Ghetto langu’ aliyoshirikishwa na Marehemu Albert Mangwea.
Huyu ni msanii wa pili kufariki
kutoka kundi la chamber squad. Miaka miwili iliyopita kundi hilo liliomboleza
kifo cha mwenzao Albert Mangwea ‘Ngwea’ huku Mez B akiwa mstari wa mbele wakati
wa mazishi yake.
Mungu ailaze
roho yake mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment