Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete azindua rasmi jengo
la kitega uchumi mjini moshi Mradi huu ni wa ubia kati ya NSSF, Tanzania Red
Cross (TRCS), UMATI na Tanzania Girl Guides Association (TGGA). Jengo hili lina
jumla ya mita za mraba 30,050 za kupangisha.
Yapo maeneo kwa ajili ya mabenki, sehemu za maduka, hoteli, kumbi za
mikutano na maeneo ya maofisi. Hivi
vyote kwa pamoja vitasaidia kutatua tatizo la maeneo ya biashara katika
Manispaa ya Moshi
Alipokuwa
akitoa historia ya mradi huu, Mkurugenzi
mkuu wa NSSF Dr Ramadhan K. Dau alisema historia imeanzia tangu mwaka 2008
ambapo taasisi tatu zilizokuwa na viwanja vitatu vilivyoungana katika barabara
za Agakhan na Arusha zilamua kuviendeleza
viwanja hivyo kwa kuingia ubia na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. NSSF
ilikubali kutoa fedha za kutekeleza mradi huu kwa asilimia 100 na mchango wa
taasisi hizo ni ardhi.Kwa sasa jengo hili linamilikiwa na taasisi nne, ambapo
NSSF inamiliki asilimia 75 na taasisi nyingine kwa pamoja zinamiliki asilimia
25. Kila taasisi imegawiwa eneo lake kwa
ajili ya kulimiliki na kulitumia kwa jinsi itakavyoamua.
Alisema
ujenzi wa mradi huu ulianza Desemba 2011 na umechukua miaka miwili kukamilika.
Gharama za ujenzi ni shs bilioni 63.4 Hadi kukamilika.
Mhe. Rais Dr.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishikana mikono Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau,
alipowasili mjini Moshi, jana kwa ajili ya kuzindua rasmi Jengo la
kisasa la Kitega Uchumi la shirika hilo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Yakob Kidula.Mhe. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akisikiliza kwa makini maelezo ya Mhandisi Mohamed Kimbe kuhusu mradi wa Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya Rais kuzindua jengo hilo Moshi, mkoani Kilimanjaro jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dkt. Ramadhan Dau.
Mhe. Rais Dr.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Moshi, mkoani Kilimanjaro jana. Kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Bi. Gaudencia kabaka.
Mhe. Rais Dr.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la kisasa la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii mjini Moshi Kilimanjaro jana. Wengine ni Waziri wa Kazi na Ajira, Bi. Gaudensia Kabaka (kushoto kwa Rais), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhan Dau (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, Bw. Leonidas Gama.
No comments:
Post a Comment