Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh. milioni tatu kutokana
na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu,
kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.
Mechi
hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa Desemba 26 mwaka jana kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Adhabu
hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka klabu
kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.
Nayo
Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 28(4) kwa
kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto Africans
iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
kuvurugika.
Kutokana
na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao
matatu. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 28(1) inayotawala ligi
hiyo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment