HATIMAYE muswada binafsi wa
kuanzishwa Baraza la Vijana la Taifa uliyowasilishwa bungeni Oktoba 31, 2013 na
Mbunge wa Ubungo John, umepangwa kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Machi
31 mwaka huu katika Mkutano wa 19 wa Bunge linaloendelea mkoani Dododoma.
Mnyika, alisema Muswada huo ulisomwa
kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa 14 wa Bunge Disemba 21, 2013, umetokana
maoni ya wadau yalikusanywa Oktoba 2014 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Maendeleo ya Jamii.
Akizungumza kwa njia ya simu mbunge huyo alisema kuwa pamoja na malengo mengine baraza hilo pia litawezesha vijana kuanzia kwenye vijiji, mitaa hadi taifa
kuweza kuwa na vyombo vya kuwaunganisha vijana wa kike na wa kiume kwa ajili ya
maendeleo yao na ya taifa.
Alisema Kujadiliwa kwa muswada huo
ni hatua ya pekee katika historia ya harakati za vijana nchini kwa kuzingatia
kuwa Sera ya zamani ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 ilitamka kwamba
kutaanzishwa Baraza la Vijana na suala hilo
kurudiwa katika Sera mpya ya mwaka 2007.
“Natambua mchango wa vijana na
taasisi zote za vijana mlioshiriki katika maandalizi ya muswada huu, unaitwa
binafsi kwa sababu tu ndio neno linalopaswa kutumika kwa mujibu wa Kanuni za
Bunge lakini ukweli ni kwamba huu ni muswada wenu; mimi ni mwakilishi,”alisema
Mnyika.
Hata hivyo, alisema kuwa Serikali
imekuwa ikikwepa kuhakikisha kwamba matakwa hayo ya sera tajwa yanatekelezwa
kwa wakati pamoja na kuwa suala hilo
linahusu mustakabali wa maendeleo ya vijana nchini.
Aidha, Baraza hilo litafuatilia pia kwa karibu utekelezaji
wa mipango ya maendeleo ya vijana ikiwemo kuhusu ajira, elimu na sekta zingine
katika Halmashauri, Serikali kuu, katika vyombo mbalimbali vya maendeleo na
wadau wa maendeleo.
Mnyika, alisema pia Muswada huo
utawezeshwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kulipa jukumu Baraza
la Vijana kufuatilia kwa karibu utendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; kuhakikisha
kwamba fedha zinatengwa za kutosha na kufika kwa walengwa kuwawezesha vijana
kujiajiri, kukuza vipaji vyao na kushughulikia maendeleo yao kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment