Na Bryceson Mathias, Mvomero, Morogoro
CHAMA cha Wafanyakazi mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU), wamempasha Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala, wakidai, aiambie Serikali kuwa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, amefilisika, hawezi kuendesha Kiwanda, na Serikali ipeleke Mwekezaji mwingine.
Akizungumza katika Mkutano wa Wafanyakazi, akiwepo Meneja wa Kiwanda cha Mtibwa, Hamad Yahaya, Kiongozi wa TPAWU Kanda na Waziri huyo, Mwenyekiti wa Tawi la TPAWU Mtibwa, Dominick Mbasha, alisema Mwekezaji huyo ameshindwa, Serikali ipeleke Mwekezaji mwingine.
Katika Mkutano huo ambao, Waziri
Makala alitakiwa aongozane na Mawaziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Masatu Wasira,
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda, alishindwa kumaliza Mgomo huo, na Wafanyakazi kuapa kuendelea kupiga
Kambi langoni kwa mwekezaji hadi walipwe.
Mbali
ya Makala kusema Mwekezaji anapaswa kuwalipa wafanyakazi hao, alisema amemuomba
ruhusa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aende kutatua Mgomo huo, na akirejea ampe
taarifa, huku akidai Mawaziri, Wassira na Dkt. Kigoda, wameshindwa
kufika kwa sababu ya kazi Maalum.
Pamoja na Meneja Mkuu wa
Kiwanda hicho, Yahaya, kumuahidi Waziri Makala kuwa ataanza kuwalipa Mishahara wafanyakazi
hao siku inayofuata hivyo warejee kazini, Wafanyakazi waligoma kuondoka
wakidai, Meneja huyo si Mkweli, hivyo watakesha hapohapo hadi watakapolipwa.
Kwa Mara nyingine, Makala
alitaka kutumia Sarakasi alizotumia awali za kuita utitiri wa Mawaziri husika na
kero
zinazomsumbua katika jimbo lake kama alivyofanya kwenye Mauaji ya Wakulima
na Wafugaji wa Bonde la Mpunga Mgongola, ili kuwatumainisha wananchi, lakini
safari hii alikwama.
Awali aliwakokota, aliyekuwa Waziri wa mifugo Dkt. David Mathayo, aliyekuwa Waziri
wa Mambo ya ndani Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa Kilimo na
Ushirika, Mhandisi, Christopher Chiza, na yeye Makala ili kutatua Mgogoro wa
Wafugaji na Wakulima, lakini hadi leo utatuzi huo bado ni ndoto za Mchana
Maisha
ya Wafanyakazi na Wakulima wadogo wa Miwa wa Mtibwa, yamekuwa ya
ukatili na unyanyaswaji Mkubwa na kupindukia wanaofanyiwa na Mwekezaji
huyo, kiasi kwamba wanaweza kufanya kazi akawalipa anavyotaka bila
kujali utu na shida walizonazo.
No comments:
Post a Comment