WANANCHI wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro wakiwamo
wajasiliamali wadogo wamechangishana shilingi milioni tisa na kumkabidhi
Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),
Innocent Melleck (pichani) kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kugombea ubunge
katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye mji mdogo wa himo baadhi ya wananchi
hao Halid Msango, Jonas Mamuya na Aisha Mkwizu walisema kwa pamoja wananchi wa
jimbo la Vunjo bila kujali itikadi zao za vyama wamemchangia kiasi hicho cha
fedha ili kimsaidie kuchukulia fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), muda utakapofika
Katika tukio hili tumeshiriki wananchi wa jimbo hili la Vunjo kwa umoja wetu
bila kujali itikadi za kisiasa ambapo hapa pia wapo wanachama wa vyama vya NCCR
Mageuzi,TLP, CHADEMA na CCM soote
tumeshiriki katika kuchanga fedha hizi lakini pia wapo makundi mbalimbali kama
vile mama lishe, madereva wa Bodaboda, wauza mboga, na vijana wengine
wanaofanya biashara ndogondogo na wapiga debe kwenye vituo vya mabasi ya
daladala.
Aidsha wananchi wao waliafikiana kuunda kamati ya kuzunguka
jimbo zima kuhakikisha kuwa wanakusanya fedha za michango na kuhamasishana
kwaajili ya kuhakikisha Melleck anapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi
mkuu wa mwaka huu.
Katika kamati hiyo mwenyekiti ni Mzee shayo na
katibu wa mwika kuwa katibu huku katibu kata kata ya kilema kusini Shabani
Kwezi kuwa mjumbe na wajumbe wawili toka kila kata za jimbo hilo hivyo kuwa na
jumla ya wajumbe 36 katika kamati hiyo ambayo ilianza majukumu yake mara moja.
Alisema zoezi hilo liliongozwa na zaidi ya wajumbe 1000 wa nyumba 10 wa CCM na
kumtaka, Melleck kuchukua fomu ya kuwani nafasi hiyo ya uwakilishi katika
uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Bwana Melleck aliwashukuru wananchi hao kwa ujasiri mkubwa na
Imani kubwa walioonyesha kwake , nimefarijika sana kuona wananchi wenye kipato
kidogo cha fedha wanachanga kiasi hiki cha fedha na kunikabidhi ili nichukulie
fomu na mimi naahidi kutowaangusha kwa hilo, nitafanya hivyo muda ukifika,"
alisema
Alisema jimbo la Vunjo linakabiliwa na changamoto nyingi hususan ukosefu wa
ajira kwa vijana na kukosa mtetezi wa asilimia tano ya mapato yatokanayo
na Mlima Kilimanjaro ili yarudi kwa wananchi, Matatizo ya kielimu na maslahi ya
walimu,Migogoro ya ardhi na miundombinu kuwa itakuwa kipaumbele chanya mara
baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo mapema mwezi octoba mwaka huu.
Melleck ambaye ni kijana alisema kwa umoja ulioonyeshwa na wana Vunjo anaamini
kwamba utaendelea hivyo hivyo mpaka uchaguzi utakapomalizika na kuhakikisha CCM
inashinda.
Alisema amejiandaa kufanya mengi katika jimbo la Vunjo na kwamba njia pekee ya
kupita ili kupata ushindi ni kuwashirikisha wananchi wote kwa kuwa anaamini
kwamba jimbo hilo litakuwa huru kufungua fursa za kuichumi ikiwa atakuwa
mwakilishi wake bungeni.
"Vunjo kuna utajiri mwingi na kinachotakiwa ni mtu mwenye maono ya kuona
fursa ili aweze kuwashirikisha wananchi kuzifikia kwa ajili ya maendeleio yao
na watoto wao," alisema
Melleck aliongeza kuwa wananchi wanayo nafasi ya kuona na kuwachuja wagombea
wote ili waweze kupata mtu sahihi atakayeweza kuwavusha hapo walipo na kusonga
mbele kwa manufaa ya wana Vunjo wote.
No comments:
Post a Comment