1. Walengwa ni Watoto waliozaliwa kuanzia tarehe 01-01-2001 hadi 31-12-2003
2. wawe na cheti halisi cha kuzaliwa na nakala yake
3. Picha mbili za pasipoti zenye rangi ya bluu nyuma
4. Watoto waambatane na wazazi wao (Baba au Mama mzazi) au Mlezi wa kisheria yaani anayetambuliwa kwa hati za kisheria.
5. Awe na vifaa vya michezo na maji ya kunywa.
6. Usajili utaanza Jumamosi saa moja asubuhi na kumalizika saa kumi jioni
7. Unguja zoezi litakuwa Amaani Stadium
8. Pemba zoezi litakuwa Gombani Stadium
9. Majaribio yatafanyika siku ya Jumapili kuanzia saa moja katika viwanja vya Gombani na Amani (unguja na Pemba)
10. Zoezi hilo ni bure wazazi hawatozwi chochote zaidi ya kuwanunulia vifaa na maji watoto wao.
No comments:
Post a Comment