Mwenyikiti
wa Chama cha C.K.U.T, Ramadhan Semtawa. Jijini Dar es Salaam akifafanua jambo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Noel Antapa.
Msajili wa
vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi,
(kulia) akimkabidhi hati ya Usajili wa Muda wa chama cha Kijamaa na Uzalendo (C.K.U.T), Mwenyikiti
wa chama hicho Ramadhan Semtawa. Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha siasa ili kiweze kuendeshwa vizuri kwa
misingi ya utawala bora na baadae kifikie malengo yake ya kuchukua dola ni
lazima kiwe na katiba yenye misingi ya kidemokrasia.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa, Sisty Nyahoza wakati wa kukabidhi cheti
cha muda kwa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (C.K.U.T).
Alisema demokrasia ya kweli ni muhimu kuanza
kujengwa ndani ya chama kwani itawasaidia viongozi kufikia malengo waliyojiwekea.
Nyahoza alisema viongozi pia wanawajibu wa
kusoma sheria ya vyama vya sisasa ili kuepuka migongano na watendaji wa taasisi
zingine za serikali.
“Leo tumetoa cheti cha usajili wa muda kwa chama
cha C.K.U.T, tunawaomba sana viongozi wa chama hiki kukaa pamoja na wanachama wenu
ili kupeana mawazo mazuri ya kujenga chama,asitokee mmoja wapo na kusema kuwa
yeye ndiye mwenye chama, hivyo someni vizuri sheria ya vyama ili msiwe na
mgogoro na taasisi zingine,” alisema.
Naye Msajili wa Vyama vya Siasa, Mstaafu Jaji
Francis Mutungi alisema ofisi ya msajili ni taasisi hivyo itawahudumia watu
wote wanaohitaji huduma.
Mwenyekiti wa chama cha C.K.U.T Ramadhani Semtawa
alisema wameanzisha chama kwa malengo maalumu ya kurejesha nchi kwenye misingi
ya waasisi.
Alisema kumekuwepo kwa rushwa na masuala la
kidini kumechangia nchi kuyumba na
kutoka katika misingi ya kidemokrasia na utawala bora.
“Watu wanauwa kwa sababu za kidini na wengine
upoteza maisha yao kwa imani za kishirikina, lakini pia wapo watu wamekuwa
wakila fedha za serikali na awachukuliwi hatua yoyote, tunataka kuja
kuibadilisha nchi hii maana aina muelekea kwa sasa,” alisema.
Semtawa alisema kinachofanyika sasa ni kutafuta
wanachama ili waweze kupata usajili wa kudumu.
“Tunatakiwa tuwe na wanachama 2000 katika mikoa
kumi na kila mkoa mmoja inatubidi tupate wanachama 200, tumejipanda vizuri na
tunaamini kuwa tutapata usajili wa kudumu,”alisema.
Aidha Semtawa alisema awatahitaji kiongozi
yoyote kutoka katika vyama vya upinzani kujiunga na chama hicho.
No comments:
Post a Comment