Mahmoud Ahmad, Arusha
Joto la ubunge katika jimbo la
Simanjiro mkoani Manyara limezidi kushika kasi mara baada ya mkuu wa wilaya ya
Kakonko,Peter Toima kutamka ya kwamba
endapo wakazi wa jimbo hilo watamshawishi na yeye kushawishika basi
atafanya uamuzi mgumu wa kuchukua fomu kwa
niaba yao muda ukiwadia.
Toima,alitoa kauli hiyo hivi karibuni
wakati alipotembelea ofisi za gazeti la Mwananchi zilizopo katikati ya jiji la
Arusha ambapo alisistiza kuwa amekuwa akipokea maombi mengi kutoka kwa makundi
mbalimbali wilayani humo ya kumtaka achukue fomu ya ubunge mwaka huu.
“Kama watu wa Simanjiro wakifanikiwa
kunishawishi na nikashawishika ,nitatii sauti yao na nitafanya uamuzi kwa
niaba yao muda ukiwadia’alisema Toima
Alisema kuwa mara kwa mara amekuwa akijiuliza
ni kwanini wakazi wa wilaya hiyo wamekuwa wakimtaka achukue fomu ya kuwania
ubunge wa jimbo hilo na kusema amebaini chanzo kinatokana na wao kuchoshwa na
uongozi uliopo kwa kuwa hakuna mabadiliko.
Alisema kuwa anasubiri muda ukifika
atafanya maamuzi magumu kwa kuwa kitendo cha wakazi hao kumpelekea maoombi hayo
ni mapenzi yao na msukumo wao ili kukidhi mahitaji yao.
“Watu wa Simanjiro wanatamani kwamba
ningekuwa mbunge wao mimi nasema hayo ni mapenzi yao,msukumo wao ili kukidhi
mahitaji yao”alissiitiza Toima
Kiongozi huyo ambaye amefanikiwa
kuhudumu ndani ya wilaya saba nchini tangu enzi za Rais Benjamin Mkapa alisemam
kuwa jimbo la Simanjiro ni miongoni mwa majimbo ambayo yameachwa nyuma
kimaendeleo kutokana na uongozi mbovu.
Naye mbunge wa jimbo hilo,Christopher
Ole Sendeka alijibu kauli ya kiongozi huyo na kusema kuwa haoni kama mtu yoyote
akiwemo Toima anaweza kuwa tishio kwake kisiasa na kudai anawasubiri katika
uwanja wa mapambano.
No comments:
Post a Comment