April 28, 2015

KATIBA INAYOPENDEKEZWA SEHEMU YA PILI

MAMLAKA YA WANANCHI 7-(1) Wananchi ndio msingi wa     mamlaka  yote, na kwa hiyo:
                          
                                (a) Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi ambao kwa                                         umoja na ujumla wao wanamiliki na kuipatia Katiba hii uhalali.

(b) Lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa wananchi.

(c)Serikali itawajibika kwa wananchi.
(d)Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.


(2) Kwa mujibu wa Ibara hii, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia na utakaoendeshwa na kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka na Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, kwa kadri itakavyokuwa.

No comments:

Post a Comment

Pages