Katibu Mkuu wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini jana
(Jumamosi Aprili 11, 2015) kuelekea nchini Marekani ambako atakuwa na ziara ya
kikazi ya siku tisa.
Dk. Slaa katika safari
hiyo ameambatana na mkewe Josephine Mushumbusi.
Ziara hii ya siku tisa
ni mwaliko wa Gavana wa Jimbo la Indiana Mike Pence pamoja na taasisi
mbalimbali za nchini humo ikiwemo vyuo vikuu kutokana na kutambua mchango wa
kisiasa na kijamii wa Katibu Mkuu huyo na chama chake katika maendeleo ya bara
la Afrika na kipekee nchini Tanzania.
Ziara hiyo itamwezesha
Dk. Slaa kushiriki mijadala mbalimbali inayohusu uwekezaji, elimu na uongozi
iliyoandaliwa kwa ajili yake ambayo lengo lake kuu ni kuitangaza Tanzania kwa
ukamilifu wake.
Kwa malengo hayo, Dk
Slaa atafanya mihadhara (Public Lectures)
kwenye vyuo vikuu vya Purdue, Indianapolis na Marion. Sanjari na mihadhara
hiyo, Dk Slaa atakua na vikao vya mashauriano na baadhi ya Maprofesa waadhiri
wa vyuo vikuu mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya kisiasa
na maendeleo na kijamii na ushiriki wa Chadema katika siasa za Kimataifa.
Zaidi, ziara hii
itamkutanisha pia Katibu Mkuu na viongozi na watendaji wakuu wa kiserikali na
makampuni mbalimbali pamoja na taasisi kubwa za uwekezaji kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika
masuala ya uchumi na uwekezeji Barani Afrika na kwa kipekee Tanzania
........................
Deogratias Munishi
No comments:
Post a Comment