April 04, 2015

MSAMA AKABIDHI MISAADA YA SIKUKUU YA PASAKA KWA WATOTO YATIMA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa mtoto Ibrahim Issa wa kituo cha Zaidia cha Sinza jijini Dar esSalaam wakati wa hafla ya kutoa zawadi za Sikukuu ya Pasaka kwa vituo vya kulelea Watoto wanaoishi katika mazingita magumu.
 Watoto wakipokea zawadi za Sikukuu kuttoka kwa Msama.
 Heid Edwin akiopkea zawadi za Pasaka kwa niaba ya watoto wezanke.
 Charles Nyimbo akipokea zawadi za Sikukuu ya Pasaka kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions kwa niaba ya Kituo cha Malaika Kids cha Sinza.
 Asante kwa zawadi za Sikukuumungu akubariki...
 Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya watoto wakiwa na zawadi zao.

NA LOVENESS BERNARD 

Kampuni ya Msama Promotions leo imetoa misaada ya vitu mbalimbali kwa vituo 7 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Alex Msama alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu ya mapato yatokanayo na Tamasha la Pasaka.

‘’Misaada hii ni mapato ya Tamasha la Pasaka mwaka jana  ,tumewapa watoto zawadi hizi ili washiriki vema katika kusheherekea sikukuu ya Pasaka na wajisikie kama watoto wengine’’, alisema Msama.

Kwa upande wake mmoja wa walezi wa vituo hivyo Honoratha Michael ambaye ni mlezi wa kituo cha Honoratha kilichopo Temeke, alisema kuwa anaishukuru  Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwapa misaada hiyo wanaomba nawatu wengine wajitolee kuwasaidia.

‘’Tunamshukuru Msama na kampuni yake na hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea Baraka kutoka kwa Mungu baba pia tunawaomba watanzania wengine wajitolee kwani tunazo changamoto nyingi katika vituo vyetu’’alisema Honoratha.

Misaada hiyo iliyotolewa jijini Dar es Salaam imegharimu million sita imewanufaisha watotowa vituo vya Honoratha (Temeke),Malaika kids (Kinondoni), Umra(Magomeni),Mwandaliwa( Boko), Zaidia (Sinza) na kituo cha Rahman kilichoko Magomeni.

No comments:

Post a Comment

Pages