April 24, 2015

TEA YAKABIDHI VITABU VYA KIADA KWA SHULE MSINGI 48 ZA MIKOA YA DAR NA PWANI

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majdi Mwanga (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vitabu vya kiada kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent vilivyotolewa na Kampuni ya Oxford University Press kwa  ajili ya Shule za Msingi 48 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Bagamoyo juzi. Wa pili kulia ni Meneja Mkuu wa Oxford, Fatma Shangazi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Respicius Selestin. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia hafla ya ugawaji wa vitabu kwa Shule za Msingi.
Wanafunzi wa Shuleya Msingi Majengo wakisaidia kupanga vitabu.
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe (kushoto) akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo ya Bagamoyo wakiandaa vitabu vilivyotolewa kwa shule za msingi 48 katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majdi Mwanga akizungumza katika hafla hiyo. 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo akizungumza katika hafla hiyo.
Burudani ya ngoma.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jitegemee wakitumbuiza kwa ngoma za asili.
 Sarakasi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo wakionyesha vipaji.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo iliyopo Bagamoyo, Munzili Feruzi akionyesha umahiri wa kuruka sarakasi wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu kwa shule za msingi 48 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani iliyofanyika mjini Bagamoyo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu vya kiada kwa Shule 48 za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majdi Mwanga (wa pili kushoto) akimkabidhi kitabu cha kiada mwanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo, Moza Mketo baada ya kupokea msaada wa vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya Oxford University Press kwa  ajili ya Shule za Msingi 48 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Bagamoyo juzi. Kulia ni Meneja Mkuu wa Oxford, Fatma Shangazi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Respicius Selestin.

No comments:

Post a Comment

Pages