April 09, 2015

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WASHIRIKI WA MKUTANO MKUU WA 31 WA ALAT

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko (UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliono. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.
Mifuko hii huwawezesha wawekezaji kuweka akiba na kuwekeza fedha zao na zikakua zaidi.Hatimaye huwawezesha kufanya uwekezaji zaidi katika shughuli za ujasiriamali,kupeleka watoto shule au kufanya shughuli zozote za kiuchumi.
Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye zaidi ya thamani ya Shilingi bilioni 235.
Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo  muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns).  Wawekezaji wote wananufaika  kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.
Ofisa Masoko na Uhusiano UTT AMIS, Rahim Mwanga,  akitoa maelezo kuhusiana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS kwa Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia (kushoto)  na  Naibu Waziri TAMISEMI, Aggrey Mwanri wakati wa Mkutano Mkuu wa  31 wa ALAT. 
 Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akisaini kitabu cha wageni katika banda la UTT AMIS.
 Naibu Waziri wa Elimu, Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni.  
Mmoja wa watu waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 31 wa ALAT akipata maelezo kuhusiana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja kutoka kwa Ofisa Masoko na Uhusiano UTT AMIS, Rahim Mwanga. Katikati ni Ofisa wa UTT AMIS, Waziri Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

Pages