June 30, 2015

Diwani afanikisha Magaidi watatu kukamatwa

  • Adai walikuwa na SMG, Risasi 50, Jambia na Mabomu
  • Na Bryceson Mathias, Kibindu
DIWANI wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mfikilwa Mkufya (CCM), alimaarufu Mawazo, amefanikisha kukamatwa kwa Magaidi watatu wakiwa na Silaha (SMG), Risasi 50, Mabomu, Jambia moja, Vipande 45 vya Nondo fupi, na Baruti, mara tu walipopanda Basi Kito cha Kwaluhombo.
Diwani Mkufaya ndiye aliyekuwa Shujaa aliyewabaini Magaidi hao walipopanda Basi la Passion T328 DEY  lililokuwa likiendeshwa na, Seleman Ally, na Utingo, ,Juma Seleman, linalofanya safari zake kati ya Kibindu na Dar es salaam, wakiwa na Kifurushi cha Kilo 25, kilichosadikiwa kuwa na vitu vya hatari.
Mkufya alisema, yeye alikuwa ndani ya Basi hilo akitoka Kibindu kwenda Lugoba, ila walipopanda Magaidi hao kijijini hapo na Kifurushi, alimshitukia mmoja aliyekuwa kama Msomali, akasubiri eneo lenye Mtandao, atoe taarifa Polisi.
Diwani Mkufya alisema, walipofika eneo lenye Mtandao alitoa taarifa Polisi, ambapo Askari wa Mbwewe waliwakamata na kuwafunga Kamba baada ya kuona ni watu hatari, na kwenda nao Chalinze, ambapo walipopekuliwa, Mkufya anadai walikutwa na Silaha ya SMG, Risasi 50, Nondo upi 45, Jambia lililoandikwa Al-shabaaby, na Baruti za kutegea mabomu.
"Nimeambiwa na mwenzangu aliyeelekea mpaka Chalinze, wale watu walpekuliwa na kukutwa na Silaha ya SMG, Risasi 50, Nondo fupi 45, Jambia moja lililoandikwa Al-shabaaby, na Baruti za kutegea Mabomu.
Mapema aubuhi ya leo, Tanzania Daima lilimuuliza Mtendaji wa Kijiji cha Kibindu, Juma Mhagama, hali ikoje siku ya kuamka leo, na ndipo aliposema, Diwani wa Kata ya Kibindu, Mkufya, aliwashitukia Magaidi watatu waliopandia Basi Kituo cha Kwaluombo, na kutoa taarifa Polisi.

Aidha Mkufya alisema, Magaidi hao hivi sasa wanakimbia ovyo katika Msitu wa Kata yake wakihangaika kujinusuru na Msako wa Vyombo vya Usalama na Wananchi, ambao amedai  wameelimishwa vya kutosha kulinda nchi yao, na wakiona kitu wanatoa taarifa mara moja, hivyo anawaomba waendelee na Moyo huo.

No comments:

Post a Comment

Pages