Bi. Chikulupi Njelu Kasaka
Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Mbeya Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) akikabidhiwa Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Mbeya na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu
Kushoto ni Bw. Moses Mwakibinga Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Chunya, Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu Baada ya kukabidhiwa Fomu
MFAHAMU BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA
*Anaitwa Chikulupi Njelu Kasaka.
*Ni Mwanasheria (wakili) kitaaluma.
*Ni mfanyakazi wa Bunge la JMT
.
*Sasa anawania Ubunge wa Viti-maalum (vijana).
*WASIFU WA MGOMBEA: BI. CHIKULUPI KASAKA
ELIMU:
Chikulupi Kasaka ni mzaliwa wa Chunya na babu na Bibi ni wakazi wa Kijiji cha
Mtanila katika Wilaya ya Chunya.
Chikulupi alizaliwa mwaka 1986 na kuanza elimu
ya msingi mwaka 1994 katika shule ya Chunya Kati. Chikulupi alimaliza elimu ya
msingi Mkoani Tabora na kuchaguliwa kwenda shule ya Serikali ya Sekondari ya
Wasichana Msalato iliyopo Dodoma ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne
mwaka 2000-2004. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Shule ya Serikali ya Sekondari ya
Wasichana Loleza iliyopo Mkoani Mbeya. Alishaguliwa kijunga na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam mwaka 2007 kusomea Shahada ya Kwanza ya Sheria na kumaliza mwaka
2011. Mwaka 2013 alijiendeleza kwa kujiunga na mafunzo ya uanasheria kwa vitendo
na kumaliza mwaka 2014 katika chuo kiitwacho Law School of Tanzania ambapo
baadaye niliapishwa kuwa wakili.
UZOEFU KATIKA UONGOZI:
Chikulupi aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwa anasoma Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam. Alikuwa Mbunge katika Serikali ya wanafunzi - DARUSO.
Chikulupi alichaguliwa mwaka 2009 kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa
Afrika Mashariki uitwao East Africa Community Students Union -EACSU.
Pia
alikuwa Afisa Mahusiano ya Umma katika Taasisi ya wanafunzi wa Sheria iitwayo
University of Dar es Salaam Human Rights Association –UDHRA. Mwaka 2010
alishiriki mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yaliyofadhiliwa na Shirika la
Kijeruman liitwalo Friedrich Ebert Stiftung –FES.
Pia mwaka 2014 alishiriki
mafunzo ya Viongozi Vijana toka barani Afrika nchini Marekani ambao alisomea
masomo ya Public Management katika chuo cha Howard kilichopo Washington. Pia
nilipata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama ambae ni mwanzilishi wa mafunzo
haya.
UZOEFU NDANI YA CHAMA/UVCCM:
Chikulupi Kasaka alijiunga na CCM hasa katika jumuiya ya UVCCM mara tu baada ya
kumaliza elimu ya sekondari 2006.
Alipokuwa anasomea Shahada ya Sheria Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam alijikita katika shughuli mbalimbali za kuimarisha
chama na mwaka 2010 alichaguliwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi ya Abiyan-Chuo Kikuu.
Na mjumbe wa Shirikisho la Vyuo Vikuu wanaCCM, Mkoa wa Dar es Salaam.
KAZI:
Mara baada ya kumaliza chuo kikuu Julai 2011 Chikulupi alifanya kazi katika
Shirika la Wakimbizi katika Mradi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uitwao
International Migration Management Program (IMMP).
Mwaka 2012 aliajiriwa na
Serikali kama Hakimu Mkazi daraja 2, katika Mahakama ya Mwanzo
Makongorosi-Chunya, Mbeya. Mwishoni mwa mwaka 2012 nilijiunga na utumishi wa
Chama Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Nilipangiwa kufanya kazi za Chama katika
Upande wa Bunge hasa za kisheria. Tangu kipindi hicho mpaka sasa Chikulupi
anafanya kazi kama Msaidizi wa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, Bungeni Dodoma.
VIPAUMBELE:
Chikulupi Kasaka anaomba ridhaa yako ili aweze kuwawakilisha vijana wa Mkoa wa
Mbeya katika nafasi ya Uongozi wa Kitaifa kupitia ngazi ya Ubunge wa Viti
Maalum-Vijana.
Kama mkazi wa Mbeya naamini vijana wa Mbeya wanauwezo, nguvu,
bidii na jitihada katika shughuli zao za kila siku. Lakini mimi nitapigania kuwapatia
vijana wa Mbeya fursa nyingi zaidi katika vipaumbele vifuatavyo:
ELIMU, AJIRA,
MICHEZO, UTALII na AFYA.
ANAOMBA UMUUNGE MKONO KWA FURSA ZAIDI KWA VIJANA WA MKOA WETU WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment