July 10, 2015

Diwani Tunduma awaaga wananchi


NA KENNETH NGELESI, TUNDUMA


DIWANI aliyemaliza muda wake katika Kata ya Tunduma kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Frank Mwakajoka (pichani) amewaaga wananchi wa kata hiyo huku akiwaasa wananchi kuwaenzi watumishi serikali katika idara mbalimbali ikiwemo Sekta ya elimu ili kusaidia kumaliza matatizo yaliyopo.


Wito huo imetolewa hivi karibuni na Diwani huyo katika mkutano wa hadhara ambao ulikuwa kwa ajili ya kuwaaga wananchi wa kata hiyo uliofanyika Uwanja wa shule ya Msingi Mwaka mjini Tunduma,ikiwa ni siku tano tangu baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Mbeya kuvunjwa.


Mwakajoka alisema kuwa ni vema wananchi wakatoa ushirikiano wa hali na mali kwa watumishi hasa katika sekta ya elimu ili kuweka mazingira mazuri ya watoto kupata elimu kwa lengo la kata hiyo kuwa na maendeleo ya kudumu katika kipindi hiki ambapo hakutakuwa na uwakilishi.


Akizungumza na mamia ya wananchi walifurika uwanjani hapo Mwakajoka alisema Tunduma bado kuna unakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa nyumba za walimu, hali ambayo inawafanya watumishi hao kutofanya kazi zao kwa utulivu hivyo ni vema wananchi wawe na ushirikiano mzuri na watumishi hao ambao wanajukumu zito la kutoa elimu bora kwa watoto wao hivyo ni kwao kusaixdia na Serikali kutatua changamotop hizo ikiwemo ya n yumba za walimu.


“Ndugu zangu hawa walimu siyo kwamba kule waliko toka hawahitajiki la hasha,bali wapo hapa kwa mjibu wa sheria lakini pia ndugu zangu wanatunduma ni wajibu wetu kutoa ushirikiano kwao siyo kwa walimu tu bakli pia hata kwa watumishi wa sekta nyingine ambao wapo hapa kwa jili kututumikia sisi lakini na taifa kwa ujumla’alisema Mwakajoka.


‘Na ili tuweze na maendeleo endelevu ni lazima tuwaenzi walimu’ wanaowafundisha watoto wetu, kwani tumefanya kazi kubwa ya kujenga vyumba vya madarasa na kununua madawati, lakini bado walimu wetu wanachangamoto kubwa ya kupata nyumba za kuishi, nawasihi tuwaenzi na kutoa ushirikano kwa walimu hawa kwa kutatua changamoto zao,” aliongeza  Mwakajoka.


Aidha katika hatua nyingine akizungumzia maendeleo ya mji wa Tunduma, Mwakajoka alisema kuwa wakati akiingia madarakani alikuta ukusanyajiwa mapato ukiwa wa chini huku ikitengwa bajeti ndogo ya maendeleo ya kiasi cha shilingi milioni 800.

Alisema amekuwa akijitahidi kuibua vyanzo vipya vya mapato na kudhibiti vilivyopo hali ambayo imeongeza mapato na bajeti ya mji huo hadi kufikia zaidi ya shilingi  bilioni 1.8 kwa mwaka.


Mwakajoka alisema kuwa kutokana na jitihada hizo, zilipatikana fedha ambazo ziwezesha kujengwa kwa barabara nzuri kwa kiwango cha lami, changalawe, na kuanzisha barabara mpya ambazo hazikuwepo kabla ya yeye kuingia madarakani.


Aidha alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanikiwa kujenga madaraja katika maeneo mbalimbali, barabara nyingi, vyumba vya madarasa, visima vya maji, maabara kwenye shule za sekondari, vituo vya afya na zahanati.


Diwani Mwakajoka alisema kuwa pia amefanikiwa kupandishwa hadhi kwa mji wa Tunduma ambao ameingia madarakani ukiwa ni kata, lakini sasa anapostaafu mji huo umekuwa Halmashauri kamili inayojitegemea.


Alisema kuwa kwenye uchaguzi Mkuu ujao kata ya Tunduma pekee itagawanywa katika kata 12 na nyingine tatu za pembezoni mwa mji zitaongezwa na kuifanya Halmashauri ya Mji wa Tunduma kuwa na kata 15.


Aliwataka wananchi wa Tunduma kuichagua Chadema kwenye kata zote ili kukiwezesha chama hicho kuunda halmashauri ambayo itaendeleza mambo mema aliyoyaanzisha na kuyaacha kabla hayakamilika.


 Alisema mpaka anastaafu ameacha bajeti ya ya Halmashauri hiyo ya shilingi bilioni 22 ambazo zitatumika kuleta maendeleo kupitia kwenye miradi mbalimbali.

Kwa upande  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chadema, Harod Jivava alisema kuwa baada ya kazi nzuri ambayo imefanywa na diwani huyo, sasa nia ya chama hicho ni kupata madiwani wengi zaidi wakatakaounda Hamlashauri ya mji wa Tunduma kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages