JESHI la Polisi limesema, Hali ya Ugaidi iliyokuwa inawatishia Wananchi wa Kata ya Kibindu wilayani Bagamoyo hasa vijiji vya Pera, Kwaluhombo na Njeura mpakani mwa Mvomero, sasa ni Shwali
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, alikiri kwamba kwa ujumla hali ni shwali. "Kwa ujumla baada ya Kamatakamata ya Magaidi hao iliyotokana na ushirikiano na wananchi, na wananchi warejee kufanya shughuli zao za Kiuchumi bila hofu".alisema RPC Mohamed.
Mtendaji wa kijiji cha Kibindu, Juma Mgaza, pia alikiri akisema hali ni sasa ni shwali na wakulima wamerejea mashambani kuendelea na shughulizakilimo.
Naye Mtendaji wa Kijiji cha Pera, Mwanahawa Mabwani alisema, "Tunalisjikuru Jeshi la Polisi na Ushirikiano mzuri uliotolewa na Wananchi kwa kufichua na kutoa taarifa za Magaidi hao na kukamatwa".alisema.
Katibu Kata ya Kibindu, Godwini Mhagama, alisema narejea toka safari ya Bagamoyo niliyokwenda kikazi, lakini hali ya hofu ya Magaidi sasa itakuwa historia kutokana na ushirikiano wa kuwatokomeza uliooneshwa.
Diwani wa Kata hiyo, Mawazo Mkufya, alisema, "Nawaomba wananchi, umoja tuliouonesha kutoa taarifa kwa Polisi dhidi ya Magaidi waliotaka kutuangamiza na kutugawa, huohuo utumike kujitokeza kwenye uandikishaji wa BVR ili Oktoba 25, utumike kuchagua viongozibora.
Hata hivyo mwandishi aliwaona baadhi ya Askari ambao wamebaki katika vijiji ambao wamebaki wakiendelea na ulinzi wakishirikiana na wananchi, huku uandikishaji wa vijana kwaajili ya mafunzo ya mgambo ukiendelea.
No comments:
Post a Comment