July 08, 2015

Magaidi watelekeza risasi 50

Na Bryceson Mathias, Kibindu

KUTOKANA na Msakao Mkali wa Magaidi uliokuwa ukiendelea kwenye Vitongoji na Vijiji vya Kibindu, Pera, Kwaluhombo, Negelo na Vitongoji vinavyozunguka eneo hilo la Mapigono, Magaidi waliojificha porini, wamelazimika kutimka na kutelekeza Vitabu, Sare, na Risasi 50 za Shortgun shambani.

Mtendaji wa Kijiji cha Kibindu, Juma Mgaza, amesema, kutokana na Msako Mkali unaoendelea katika Vitongoji na Vijiji ambavyo vilivamiwa na Maharamia hao, Juzi baada ya kuzidiwa Mbinu walilazimika kukimbia na kuteleza Vitu hivyo shamabani.

Alivitaja vitu hivyo kuwa ni, “Sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) (2), Bomu lililotengenezwa (1), Risasi (50) za Bunduki (Shotgun),Fulana (3),Vitabu vya Koran (2), Kisu-Jambia (1) na Begi (1), ambavyo vilifikishwa Polisi. alisema Mgaza.

Polisi mkoani Pwani imethibitisha kuokotwa kwa Vitu hivyo shambani, hivyo wamewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwa makini kuokota vitu kama Bomu wasivyovielewa isipokuwa watoe taarifa maeneo waliyotaarifiwa.

Habari toka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Pera,Mwanahawa Makani amesema, kuna watu wawili leo wamekuwa wakioneka kwenye Kisima cha Maji shambani kwa mwananchi mmoja, hivyo kuwafanya watu hasa akina Mama kuwa waoga kwenda kuchota Maji, lakini Polisi wa eneo la tukio wamesema, Jambo hilo linafanyiwa kazi.

Hata hivyo kulikuwa na taarifa zilizozagaa kwamba, katika Kijiji cha Pera kuna Wananchi watatu wameuawa na Magaidi, lakini habari hizo zimekanushwa na Mtendaji Mwanahawa, akisema, Kuna Magaidi Wawili ambao walikuwa wakingoja Wananawake kwenye Kisima.

Mwanahawa alipoulizwa iwapo wananchi wanajitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kuduma la Wapiga Kura, Mwanahawa alisema, “Watu wamejitokeza kwa Wingi na Wanaendelea kujitokeza bila Woga wa Changamoto ya Magaidi hao, isipokuwa Mashine ndizo zinawaangusha hazina Mtandao.

Wananchi waliohojiwa kwa Nyakati tofauti akiwemo, Mama Judith Kamwana wamesema, “Hatuogopi kujiandikisha kwa sababu ya Magaidi kwa sababu ua Ulinzi ambao Tangu awali tumeshuhudia, Polisi ikishirikiana Vizuri na Viongozi na Wananchi, kutoa taarifa kila jambo la ajabu linapotokea”.alisema Kamwana akiungwa Mkono na Wenzake.

No comments:

Post a Comment

Pages