Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akiwa amenyanua juu DVD, kama ishara
ya uzinduzi wa albamu ya ‘Jipange Dunia’ ya Kwaya ya Mt. Cecilia mjini Dodoma juzi.
(Picha na Danson Kaijage)
NA
MWANDISHI WETU, DODOMA
MKURUGENZI
wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, mwishoni
mwa wiki alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa DVD za albamu ya ‘Jipange
Dunia’ ya Kwaya ya Mt. Cesilia ya Parokia ya Mt. Maria Imaculata.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika katika kanisa hilo
lililopo eneo la Bihawana, nje kidogo ya mji wa Dodoma,
Msama mwasisi wa matamasha ya muziki wa injili nchini, alitoa wito kwa wenye
kipaji kuitambua talanta yao.
Msama
alisema kazi ya uimbaji ni wito na ni huduma ambayo inatolewa na waimbaji kwa
ajili kusaidia roho za watu zisipotee kwa kuishi maisha ya mema ya kumtumaini
na kumpendeza Mungu kama vitabu vitakatifu vinavyoagiza.
Aidha,
Msama alikubali ombi la Kwaya hiyo kuwa mlezi akisemo hiyo ni heshima kubwa
kwake kwani imeonesha ni kwa jinsi gani walivyomthamini kuanzia suala la kumpa
heshima ya kuwa mgeni rasmi.
‘’Nimekubali
kuwa mlezi wa kwaya hii,ninashukuru kwa kunidhamini na kunialika kuwa mgeni
rasmi,mimi nipo Dar es salaam lakini mmenialika mimi na kuwaacha watu wengi
hapa Dodoma,’’ alisema Msama na kuongeza:
‘’Nimekuja
kusaidia kwa sababu kutoa sio utajiri wala sina mali nyingi, ila namtumikia Mungu
kwa njia hii kwa kuwa ninajua nilipotoka,’’ alisema Msama mmoja wa watu wenye
moyo wa kusaidia makundi mbalimbali katika jamii kama yatima, walemavu na
wajane.
Awali,
akisoma risala, Exaveli Sudai alisema kwaya hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi
ikiwemo kukosekana kwa fedha pamoja na vitendea kazi vya uimbaji na kuomba
sapoti zaidi ili waweze kufikia malengo ya kuhubiri injili ya Mungu.
Mbali
ya Msama kutoa kiasi hicho, pia aliendesha harambee iliyozaa matunda ya
kupatikana sh. milioni 3.4 na ahadi sh. mil
1.3, hivyo fedha taslimu na ahadi kufikia jumla ya shilingi mil 4.7.
No comments:
Post a Comment