July 08, 2015

UTT AMIS YASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA 39 NA KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI KWENYE MIFUKO YA PAMOJA KWA WANANCHI

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliono. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.

Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya Zaidi ya Shilingi bilioni 237.


Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo  muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns).  Wawekezaji wote wananufaika  kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisikiliza na kufurahia maelezo kutoka kwa Bi Martha Mashiku, Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi UTT AMIS(katikati), Kushoto ni bi Sophia Mgaya afisa mwandamizi kitengo cha Tehama na Kulia ni Bi Jesca Swai,  Mhasibu wa Mifuko inayoendeshwa na UTT AMIS
  Hapa ni rahisi tuu!!Afisa Masoko na Uhusiano msaidizi Bw. Waziri Ramadhani akimuelekeza mwekezaji jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga katika moja ya mifuko ya uwekezaji ya UTT AMIS
Tunaweza kuwasaidia kujaza fomu zenu! Bi. Pauline Kasilati na Dorice Mlenge Ofisa wasaidizi wakitoa huduma kwa wawekezaji kwa kuwasaidia kujaza fomu za kujiunga na Mfuko wa Watoto
Bw. Laurian Chokola, Afisa mwendeshaji msaidizi akiwaelekeza wawekezaji kujaza fomu za kujiunga na mifuko baada ya kuwaelimisha faida zinazopatikana kwa kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages