July 02, 2015

UTT PID yatoa huduma za uuzwaji wa fomu za viwanja

Na Mwandishi Wetu

Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) ipo kwenye Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yanayoendelea katika mabanda ya Saba saba katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa jijini.

Banda la UTT PID lipo jirani na kuingia katika banda la Wizara ya fedha upande wa kuingia kwenye banda la ukumbi wa Karume. Hivyo wamewaomba wananchi mbalimbali wameombwa kujitokeza kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwemo huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo nchini ikiwemo vile vya mradi wa katika miji ya Chalinze na Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akielezea Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka katika maonyesho hayo, alibainisha kuwa mbali na uuzaji wa fomu kwa ajili ya viwanja, pia wanatarajia kuanza kuuza kwa umma na taasisi mbalimmbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi songani-Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila Mkoani Morogoro.

Aidha, Bi Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbalimbali zitolewazo na taasisi hapa nchini.

Kwa sasa UTT PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri katika utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.

Moja ya mabango ya UTT PID katika banda lao hilo ndani ya Saba saba..
DSC_1224
Mmoja wa wananchi aliyetembelea katika banda la UTT PID, akisaini kitabu cha wageni wakati alipofika kujua shughuli mbalimbali za taasisi hiyo. anayeshuhudia kulia kwa mwananchi huyo ni Afisa Masoko wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka
DSC_1199 baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka wakati walipotembelea katika banda hilo..
DSC_1250Afisa Masoko wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka akiwa katika banda lao hilo tayari kwa kutoa huduma za taasisi hiyo kwa wananchi wanaotembelea ndani ya maonyesho hayo hayo ya 39 ya Sabasaba.
DSC_1213Mmoja wa wanasheria wa UTT PID, Bw. Lawrence Nzuki (kushoto) akitoa maelezo ya kitaalam kwa mwananchi aliyetembelea banda hilo la UTT PID, kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa hapa nchini. aliyepo mbele ni Afisa Masoko wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka.

No comments:

Post a Comment

Pages