Mchezaji Kpah Sherman wa Yanga (kulia), akijaribu kumtoka Daoud Wais Ali wa timu ya Telecom ya Djibout katika mchezo wa Kagame uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga ilishinda bao 3-0.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la tatu katika mchezo huo.
XXXXXXXXXXXXXXXXX
Mabingwa mara tano wa michuano ya Kombe la Kagame timu ya Young Africans (Yanga SC) leo imeibuka na ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya Telecom kutoka nchini Djibout, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Malimi Busungu aliyefunga mabao mawili, na Geofrey Mwashiuya aliyefunga bao la tatu kwa kombora kali umbali wa mita 20 na kupeleka kilio kwa timu ya Telecom.
Katika mchezo wa leo Yanga walipoteza penati mbili zilizopigwa na washambuliaji wake Amissi Tambwe na Saimon Msuva zilizookolewa na mlinda mlango wa Telecom Nzokira Jeef.
Baada ya ushindi huo wa leo kocha mkuu wa Yanga, mholanzi Hans Van der Pluijm amesema vijana wake leo wamecheza vizuri na ndio manaa wameweza kuibuka na ushindi huo wa mabao 3- 0.
Aidha kocha huyo amesema kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa siku ya ijumaa dhidi ya KMKM utakochezwa saa 10 kamili ijumaa, ukitanguliwa na mchezo kati ya Gor Mahia dhidi ya Khartoum utakoanza saa 8 kamili mchana.
Katika mchezo wa uliotangulia mapema saa 8 mchana, timu Khartoum ilibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya KMKM, huku katika uwanja wa Karume KCCA ya Uganda ikiibuka na ushindi wa bao 1-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.
KAGAME KUENDELEA KESHO
Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam itaendelea kesho siku ya alhamis katika uwanja wa Taifa, ambapo Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR SC watacheza dhidi ya LLB ya Burundi, mechi itakayoanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Mchezo wa kwanza utazikutanisha timu ya Heegan FC ya Somalia itakayocheza dhidi ya Al Shandy ya Sudan.
No comments:
Post a Comment