Muonekano wa Cover ya Albam ya Tunapendwa na Mungu.
Mwimbaji wa
nyimbo za injili, Bonny Mwaitege (katikati) akiimba kwa hisia moja ya nyimbo
zake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam, wakati
wa akielezea namna alivyojipanga kwa ajili ya uzinduzi wa Albam zake tatu
utakaofanyika kesho Agosti 2 Jumapili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Wengine ni waimbaji wenzake kutoka kulia ni Mchungaji Faustine Munishi, Upendo Kilahiro, Jesca na Atosha Kissava. (Picha na
Francis Dande)
Mwimbaji wa nyimbo za injili mchungaji Faustine Munishi ambaye atamsindikiza Bonny Mwaitege katika uzinduzi wa albam zake tatu siku ya Jumapili Agosti 2 katika ukumbi wa Diambond Jubilee.
Bonny Mwaitege akizungumza na waandishiu wa habari.
Mdhamini wa uzinduzi wa albam ya Mwaitege, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akiimba sambamba na waimbaji watakaomsindikiza Bonny Mwaitege katika uzinduzi huo.
Na Mwandishi Wetu
Bonny Mwaitege akizungumza na waandishiu wa habari.
Mdhamini wa uzinduzi wa albam ya Mwaitege, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akiimba sambamba na waimbaji watakaomsindikiza Bonny Mwaitege katika uzinduzi huo.
Na Mwandishi Wetu
KISHINDO cha mirindimo ya muziki wa
injili, leo kinatarajiwa kuuteka ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es
Salaam, pale mwimbaji Bonny Mwaitege atakapozindua albamu tatu kwa mpigo na
kusindikizwa na waimbaji mahiri wa ndani na nje ya nchi.
Mwaitege aliyewahi kutamba na vibao
mbalimbali nchini, alisema kwamba wapendwa watarajie
kupata burudani yenye mvuto wa aina
yake kutoka katika albamu hizo mpya kwani amejipanga vizuri kutowaangusha.
“Namshukuru Mungu kunipa kipaji cha
uimbaji kwa sababu kwangu naona ni neema tu, hivyo nimeamua kumtumikia kwa karama
hii.
“Nawaomba wapendwa wasikose, waje
Ukumbi wa Diamond kujionea uzinduzi wangu,” alisema Mwaitege wakati
akizungumzia maandalizi yake ya albamu hizo tatu ambazo ni ‘Tunapendwa na Mungu,’ ‘Mama ni Mama’ na ‘Utanitambuaje.’
Alisema kazi
hizo zenye ujumbe murua wa neno la Mungu na kurekodiwa katika mazingira bora tofauti
nchini Tanzania na Kenya, anaamini zitawagusa wengi kama au zaidi ya kazi zake zilizotangulia.
Alizitaja nyimbo zilizomo katika albamu
ya 'Tunapendwa na Mungu,' ni 'Tukiimba Mungu Anashuka', 'Mtoto wa mwenzio ni
wako', 'Safari Bado', 'Tumekuja Kukuchukua (Bibi harusi)', 'Tuko Salama', 'Moyo
wa Shukrani', 'Hakuna Ridhiki' na 'Tunapendwa na Mungu'.
Naye mwimbaji nguli Faustine Munishi
mmoja aliyetua nchini kwa ajili ya kumsindikiza Mwaitege, alisema amejipanga vizuri
kuimba nyimbo kadhaa ikiwemo kibao chake kipya kisemacho ‘Malebo sasa Kaokoka’
huku wengine kama Jesca Boniface Magupa, Atosha
Kisava na Upendo Kilahilo wakiahidi makubwa.
Kwa upande wa Alex Msama, Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions iliyodhamini uzinduzi huo, alisema maandalizi
yote yamekamilika na kuwahisi wapendwa na wapenzi wa muziki wa injili
kujitokeza kwa wingi kwani kufika kwao ndi mafanikio ya huduma hiyo ya kupeleka
mbele injili ya Mungu.
Msama anawataja waimbaji wengine ambao
watamsindikiza Mwaitege, ni John
Lisu, Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Christopher Mwahangila, Eiphraim Sekereti,
Mess Chengula, Eveline Kabwemela, Ambwene Mwasongwe na Joshua Mlelwa.
Viingilio, Msama alisema ni shilingi 10,000 kwa viti maalumu;
shilingi 5,000 kwa viti vya kawaida na watoto ni shilingi 2,000. na kuongeza
kuwa wameweka viwango vya kawaida kuwezesha wengi wafike na kuweza kulipa kuchota
baraka za Mungu.
Matukio ya muziki wa injili kuanzia yakiwamo ya uzinduzi wa
almabu, tamasha la Pasaka na Krismasi ambayo yamekuwa yakiratibiwa na Msama
Promotions tangu mwaka 2000, ndio yamesaidia kukua kwa muziki huo hadi
kuwa ajira kwa wenye vipaji na wataalamu wa muziki kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment