Watoto wa familia za wafanyakazi wa wakishindana kukimbiaMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi pamoja na familia zao (Ewura Family Day) kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Ewura wakiwa katika picha ya pamoja na familia zao.
Wakiwa katika mchezo wa Wavu.
Wakishindana kukimbia huku wakiwa kwenye magunia
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi (kulia) akishiriki na wakurugenzi wenzie kushindana kuvuta kamba na wafanyakazi wa Ewura wakati wa siku ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wakishindana katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa siku ya kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi (wa tatu kushoto) akishiriki kucheza mpira wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi pamoja na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
Waliovaa fulana za bluu wakishindana soka na waliovaa njano.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo (kulia) akishiriki na wenzie katika shindano la kukimbiza kuku.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi akifurahia zawadi ya kuku aliyemkamata katika shindano la kufukuza kuku wakati wa siku ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach.
Mwanafunzi Charles Daud ambaye ni mmoja wa watoto wa wafanyakazi wa Ewura akishangilia baada ya kushinda shindano la kufukuza kuku.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi akikabidhi kikombe kwa mmoja wa washindi wa michezo iliyofanyika siku hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi (kulia) akipokea kikombe kwa niaba ya wakurugenzi walioshinda katika mchezo wa kuvuta kamba.
Ngamlagosi akifurahia zawadi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi akikabidhi zawadi ya kikombe kwa nahodha wa timu ya ilivaa fulana ya njano iliyoishinda ya bluu katika shindano la kuvuta kamba.
Wafanyakazi na familia zao waliovaa fulana ya njano wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe hicho.
Mfanyakazi wa Ewura Rachel Kiula akifurahia kupata zawadi ya kikombe aliyopata baada ya mfanyakazi pekee aliyeshiriki katika michezo mingi iliyochezwa siku hiyo.
Baadhi ya washindi wa michezo mbalimbali wakishangilia huku wakiwa na zawadi zao.
Sasa ni wakati wa msosi
Kijana mchekeshaji Comedian akiwa kazini baada ya watu kupata msosi.
Sasa ni wakati wa watoto kufurahi.
Wafanyakazi wa Ewura na familia zao wakipata ushauri nasaha kuhusu masuala ya kulinda afya zao
Wafanyakazi wa Ewura na familia zao wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment