Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba akifafanua jambo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu
adhabu zitakazotolewa kwa waajiri wa sekta ya Umma na binafsi pindi watakapochelewesha
michango yao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Uchambuzi Sera SSRA,
Angar Mushi. (Picha na Francis Dande)
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF), umewahimiza waajiri wa sekta ya Umma na binafsi kuwasilisha
michango ya wafanyakazi kwa wakati kupitia
akaunti za mfuko huo, watakaochelewesha watapewa adhabu kwa mujibu wa sharia ya
mwaka 2008 ya mfuko huo.
Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Fidia, Masha Mshomba, alisema uchangiaji ulianza Julai mosi mwaka huu kama
ilivyoelekezwa katika Tangazo la Serikali Na 169 la Mei,2015., baada ya yeye kuteuliwa
kuwa Mkurugenzi Mkuu na Bodi ya Wathamini.
“Vifungu hivyo vya sheria
vitakavyotumika kuwabana waajiri watakaochelewesha kuwasilisha michango hiyo ni
cha 75 (2), (3) na (4) vya Sheria ya
Fidia kwa Wafanyakazi, Na 20 ya mwaka 2008,alisema Mshomba.
Mshomba alisema katika
uchangiaji huo michango ya mwezi wa saba inatakiwa kupelekwa mwezi wa nane na
ya mwezi wa nane inatakiwa kupelekwa mwezi wa tisa katika benki ya NMB (akaunti Na
20110016403,tawi la Bank House), CRDB(Akaunti Na 0150237547300, tawi la Holland House) au njia nyingine
inayokubalika na kinyume cha hapo mwajiri atapewa athabu.
Alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kutokana
na Serikali kukabilina na matatizo ya ulipaji wa fidia kwa
Wafanyakazi katika Mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali.
“Matatizo hayo ni pamoja na
kiwango kidogo cha malipo ya fidia kiwango kisichozidi shilingi 108,000 kwa
ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa
wategemezi endapo kifo kitatokea kwa
mfanyakazi husika,uchache wa mafao na urasimu kwa baadhi ya waajiri katika
utoaji wa fidia.”alisema Mshomba.
Mshomba, alisema kwa mujibu wa kifungu cha
2 cha
Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi,Na 20/2008, Mfuko huu unawahusu Waajiri
na Wafanyakazi wote katika Sekta ya Umma na sekta binafsi ,Tanzania Bara.
Aliongeza kuwa katika mwaka
wa fedha 2015 hadi 2016 viwango vya uchangiaji kwa kila mwezi ni asilimia moja
ya mapato ya Wafanyakazi kwa Waajiri wa
Sekta binafsi na asilimia 0.5 ya mapato
kwa Wafanyakazi kwa Waajiri wa Sekta ya
Umma, ambapo michango hiyo ni gharama ua Mwajiri na haipaswi kukatwa kwenye
mapato ya Mfanyakazi.
Mshomba alisema mafao yatakayotolewa na Mfuko
huu ni huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa mudana ulemavu wa kudumu, kwa
anaye mhudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushauri nasaha,gharama za
mazishi na malipo kwa wategemezi wa
marehemu.
Naye kaimu Mkurugenzi Hifadhi
ya Jamii Wizara ya Kazi na Ajira, Daudi Kaali, alisema mfuko huo unakabiliwa
nsa changamoto ya uelewa wa sheria mpya waajiri na wafanyakazi bado hawajajua
wajibu wao.
No comments:
Post a Comment