NA MWANDISHI WETU
WAIMBAJI
wanaotarajia kushambulia jukwaa la Tamasha la kuombea Amani wameanza rasmi
kujifua ikiwa ni maandalizi ya tamasha hilo linalotarajia kuanza kutimua vumbi
Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia katika mikoa mingine
10
Wakizungumza na
gazeti hili waimbaji hao, walisema kuwa wameanza kujifua kwa ajili ya Tamsha hilo ambalo
linashirikisha waimbaji mbalimbali kutoka Afrika na Uingereza.
Waimbaji hao
walisema kuwa kuwa kutokana na kwamba wataimba ‘live’, hivyo wamelazimika
kuanza mazoezi mapema kwa ajili ya siku hiyo ambayo ni maalum kwa Taifa la Tanzania .
Mwimbaji Solly
Mahlangu alizungumza na gaezeti hili kwa njia ya simu na kuthibitisha kuwa
ameshaanza mazoezi japokuwa ni mzoefu wa kuimba ‘live’ lakini kutokana na
umaalum wa tamasha hilo anaongeza zaidi vionjo ili kuendana na hadhi ya tamasha
hilo.
Naye John Lisu
alisema kuwa yeye ni kawaida yake kuimba live aliwataka watanzania kufika kwa
wingi kuona uimbaji wa tofauti katika tamasha hilo huku akisisitiza kuwa kutakuwa na nyimbo
maalumu za kuliombea taifa.
Malkia wa nyimbo
za injili nchini, Rose Muhando alisema kuwa mazoezi kwake ni muhimu kwa kuwa
kawaida yake ni kuwainua watanzania katika viti vyao ambako alisema kwa
maandalizi anayoyafanya atafanya mambo tofauti na ilivyozoeleka katika maonesho
mengine aliyowahi kuhudhuria.
Waimbaji wengine
watakaokuwepo ni pamoja na Sipho
Makhabane, Glorius Celebrations ‘Kwetu Pazuri’, Ephraim Sekeleti , Solomon Mukubwa,
Anastazia Mukabwa na Sara K.
Kwa upande wa
waimbaji mahiri wa Tanzania, ni Boniface Mwaitege, Martha Mwaipaja, Beatrice
Mwaipaja, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Joshua Mlelwa na Christopher
Mwahangila. Chanzo Tanzania Daima.

No comments:
Post a Comment