HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

September 22, 2015

‘Wagombea udiwani zingatieni elimu’


Ndg Abel Mudo, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CCM akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo ulihusisha pia wakazi wa kata ya kisarawe
Baadhi ya wakazi ya kata wa kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo wa  ajenda ya watoto ullohusisha wagombea wa udiwani kupiitia vyama vya ccm na chadema 

Mmoja wa wananchi wa kata ya kisarawe akichangia katika mdahalo wa ajenda ya  watoto kuelekea uchaguzi mkuu  ambapo ulihusisha wanafunzi na wagombea  wa udiwani wa kata hiyo 



        Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige ‘A’ iliyopo Kisarawe, Mkoa wa Pwani, Amina Joka, akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, ambao uliwashirikisha wagombea udiwani wa Kata ya Kisarawe kupitia vyama vya CCM na Chadema.

Ndg Abel Mudo ambaye ni mgombea wa Udiwani kupitia CCM akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto kuelekea uchaguzi mkuu ambapo wanafunzi wa CHANZIGE ,na kisarawe 

Mmoja wa wanafunzi wa shule msingi CHANZIGE A akifuatilia kwa makini mdahalo wa ajenda ya watoto uliowahusisha wagombea wa udiwani wa vyama vya chadema na CCM 

Ndg .Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na wanafunzi



Picha za Wanafunzi ni za wanafunzi wa shule za msingi Chanzige A, Chanzige B na Kibasila zilizopo Kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo huo.

Ndg .Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na wanafunzi.



NA MWANDISHI WETU, KISARAWE


WAGOMBEA udiwani wa Kisarawe wametakiwa kueleza namna watakavyosaidia wanafunzi wa kata hiyo kuepukana na tatizo la usafiri kwa kuwajengea mabweni.

Wakizungumza wakati wa kipindi cha redio cha ‘Walinde Watoto’, kilichoandaa mdahalo uliowahusisha wagombea udiwani wa Kisarawe, Abel Mudo (CCM), Baraka Musa (Chadema) na wakazi wa Kisarawe walijadili changamoto zinazowakabili wanafunzi na mipango ya kuzitatua.

Amina Joka, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige ‘A’ alisema wanafunzi wanapata shida ya usafiri, hali inayowaathiri kitaaluma huku wazazi na viongozi walioshiriki mdahalo huo wakitaka wagombea hao kuzingatia elimu kwa watoto.

Akinadi Ilani ya Chadema, Musa alisema chama chao kinaamini kuwa lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu na kuahidi kuwekeza kwenye kupata Katiba itakayotambua na kutaja haki za watoto.

Mudo wa CCM alisema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi kitawekeza katika shule na kuhakikisha zina walimu wa kutosha na mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment

Pages