HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2015

WABUNGE WATEULE WAWASILI MJINI DODOMA

Wabunge wateule Kasim Majaliwa (kushoto) na Goodluck Ole Medeye (katikati) wakisalimiana walipokutana kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju. Vikao vya bunge viaanza Novemba 17. (Picha na Said Powa)
Wabunge wateule wa Chadema Joseph Mbilinyi (sugu) Mbeya Mjini na Joseph Haule (Profesa Jay) Mikumi wakiingia kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma kukamilisha taratibu kabla vikao vya bunge. 
 Mgombea wa kiti cha uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM, Job Ndugai (watatu kulia) akishangilia na kupongezwa na wabunge wenzake mara baada ya kupita bila kupingwa kuwania nafasi hiyo baada ya wagombea wenzake kujitoa mjini Dodoma.
 Katibu wa bunge Thomas Kashilila akizungumza na waandishi wa habari kuhusu idadi wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge waliojitokeza mjini Dodoma, ambapo wagombea wanane kutoka ndani ya vyama wamejitokeza.
 Wabunge wateule wakiwa ndani ya ukumbi wa bunge jana jioni kwaajili ya maelekezo mbalimbali ya maandalizi ya mkutano wa kwanza wa bunge la 11 mjini Dodoma unaoanza Novemba 17
 Baadhi ya wabunge wateule wa CCM waliojitokeza kumpigia kura mgombea wa uspika wa chama hicho mjini Dodoma.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee akisalimiana na wabunge wapya kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dooma jana walipoingia kwa ajili ya maelekezo mbali mbali kujiandaa na mkutano wa kwanza wa bunge la 11 linaloanza Novemba 17. 
Wabunge wateule Kasim Majaliwa (kushoto) na Goodluck Ole Medeye (katikati) wakisalimiana walipokutana kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Kulia kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju.
Aliyekuwa mgombea wa uspika CCM ambaye alijitoa kumwachia Job Ndugai, Abdullah Hussein Mwinyi (kulia) akipongezwa na wabunge wenzake baada ya kjitoa na kumwachia ndugai.

No comments:

Post a Comment

Pages