Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Ramadhan Mungi akionesha Bunduki aoina ya Short Gun iliyokamatwa ikiwa imefichwa katika tundu la Choo katika eneo la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Ramadhani Mungi akizungumza na wanahabari kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni.
Na Dixon Busagaga wa Globuu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini
JESHI la Polisi
mkoani Kilimanjaro linawashikilia wa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio
mbalimbali likiwemo la mauaji pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha
yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.
Mbali na
watuhumiwa hao Polisi pia imefanikiwa kukamata Bunduki aina ya shortgun (Pump
Action) yenye namba 69901 ikiwa imefichwa katika tundu la choo nyumbani kwa mmoja
wa watuhumiwa hao eneo la
Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.
Bunduki hiyo pamoja na risasi tatu imetajwa kukodishwa na watuhumiwa na kisha kutumika katika
shughuli za kihalifu ikiwemo uporaji wa fedha katika maeneo tofauti na mali
huku ikihusishwa pia kufanya mauaji.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Kilimanjaro,Kamishina msaidizi wa Polisi, Ramadhani Mungi alithibitisha
kukamatwa kwa watu hao pamoja na bunduki na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani upelelezi utakapo kamilika.
“Katika siku za
mwisho wa Desemba mwaka jana na siku za mwanzoni za mwaka huu ,kulikuwa na
wimbi la matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya Short gun ambayo pia
ilisababisha mauaji,tayari tumewakamata watu kadhaa na jana (juzi) asubuhi
tuliweza kuikama silaha aina ya Short gun.”alisema Mungi.
Wakati huo huo matukio
ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameendelea kushika kasi
mkoani ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa ) alikatwa
matiti yote mawili baada ya kujinasua katika jaribio la kubakwa.
Kamanda wa Polisi
mkoani hapa,Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja
mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo kuwa ni Anold Josephate ambaye alitoweka na
matiti hayo baada ya kuyaweka katika mfuko wa plastiki.
Alisema tukio
jingine linalo ashiria kuongezeka kwa makosa ya unyanyasaji na ukatili wa
kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni tukio la juzi ambapo mwanamke mmoja
aliyfahamika kwa jina la Vailet Apiniel ameuawa baada ya kunyongwa shingo.
“Siku za karibuni
hapa yamejitokeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanayo uaibisha mkoa wetu,matukio
ya ubakaji,matukio ya watu kutupa vitoto,haa ni matukio mabaya na jana tu kuna
mwanaume aitwaye Denis Shayo alimnyonga mke wake”alisema Mungi.
Alisema eneo hili
linahitaji kutolewa elimu ya kutosha huku akizitaka taasisi zinazojishughulisha
na utetezi wa masuala ya kijinsia kushirikiana na jeshi la polisi katika
kupambana na matukio kama hayo.
No comments:
Post a Comment