Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za mchezo wa netiboli za CDA Dodoma na Uchukuzi
SC jana ziliendeleza ubabe kwa kuwafunga wapinzani wao bila huruma kwenye
mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
CDA Dodoma inayoundwa na wachezaji wazoefu
iliwafunga TPDC kwa magoli 38-12. Washindi walikwenda mapumziko wakiwa mbele
kwa magoli 21-6.
Nao wadada machachari wa Uchukuzi SC wakiongozwa na
kocha wao maarufu, Judith Ilunda waliwafunga Tanesco kwa magoli 31-13. Hadi
mapumziko washindi walikuwa mbele kwa magoli 19-5.
Wafungaji mahiri wa Uchukuzi SC, Matalena Mhagama
alipachika magoli 17 na Grace Mwasote magoli 14, huku Caltace Monampo wa
Tanesco alifunga matano na mwenzake Sandra Mfaume magoli nane.
Katika mchezo wa soka, timu ya Uchukuzi SC
iliwahenyesha Geita Gold Mine (GGM) na kutoka sare ya bao 1-1. GGM ndio
walioanza kupata bao dakika ya 33 kwa mshambuliaji wake Oswald Binamungu
aliunganisha krosi ya Quentin George, na Ramadhani Madebe aliyekuwa akihaha
uwanja mzima kusaka bao aliisawazishia Uchukuzi katika dakika za nyongeza.
Katika mchezo mwingine wa soka, timu ya Ukaguzi
waliwachapa wenyeji CDA kwa magoli 4-1. Victor Ngalawa ndio alikuwa wa kwanza
kuandika bao katika dakika ya sita, na Pemsi Msenga alisawazisha katika dakika
ya 18.
Ukaguzi waliendelea kuwashambulia CDA na Deo Masanja
(mchezaji wa zamani wa Simba SC) aliongeza bao la pili katika dakika ya 33,
huku Ally Mpondo alifunga la tatu dakika ya 82 na Yahya Salum alifungala nne
dakika ya 89.
Katika mchezo wa riadha mbio za marathoni wanaume
ameshinda Atson Mbughuni wa Tamisemi kamaliza kwa 0:35.32, wapili ni Lazaro
Lugano wa tanesco katumia 0:42.45 na watatu ni Ramadhani Wakilongo wa Uchukuzi
SC katumia 0:48.17.
Upande wa wanawake riadha alishinda Stella Mroso wa
TPDC kwa 0:42.36, huku wa pili ni Beltila Genadius wa Tamisemi kwa 0:44.00 na
watatu ni Scholastica Halisi wa Uchukuzi kwa 0:49:21.
Katika michezo ya jadi kwa upande wa karata wanawake
bingwa ni Sheila Mwihava wa Tanesco alimshinda Mayasa Kambi wa UDOM katika
fainali na mshindi wa tatu ni Bupe Munisi wa Mawasiliano, kwa upande wa wanaume
ametwaa ubingwa Haji Chilo wa UDOM, huku wa pili ni Omari Said wa Tanesco na
watatu ni Ally Zongo wa Uchukuzi SC
Mshambuliaji Ramadhani Madebe wa Uchukuzi SC akikokota mpira katikati ya uwanja, huku Mohamed Salum wa GGM akimsogelea. Timu hizo zimetoka satre ya bao 1-1.
Scholastica Halisi wa Uchukuzi SC akimaliza mshindi wa tatu wa mbio za marathoni kwa kutumia muda wa 0:49.21.
Ramadhani Mwalongo wa Uchukuzi akimalizia mbio za marathoni kwa wanaume na kuibuka mshindi wa tatu kwa kutumia muda wa 0.48:17.
Ally Zongo wa Uchukuzi SC (kushoto) akiokota karata dhidi ya Kelvin Gadi wa TPDC.
Mayasa Hamidu (C) wa Uchukuzi SC akiangalia wa kumrushia mpira huku Nathereth Mwanjala (WA) wa Tanesco akisogea kumuwahi . Uchukuzi aliibuka washindi kwa magoli 31-13.
Prisca Ferdinand wa Uchukuzi SC (kulia) akilamba karata mbele ya mpinzani wake Theodora Stanslaus wa Ujenzi katika mashindano ya Mei Mosi.
Issack Ibrahim (mwenye mpira) akimtoa Fernand Makanga wa GGM akimzuia asilete madhara. Timu zilitoka sare 1-1.
No comments:
Post a Comment