April 26, 2016

WANANCHI TABATA KIMANGA WAPANGA MIKAKATI YA KUJILINDA

 WANANCHI wametahadharishwa kwamba wanaweza kufungwa ama kulipishwa faini iwapo watashindwa kutoa michango kwajili ya ulinzi shirikishi iwapo mkutano wa mtaa ukipitisha kulipwa kwa michango hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Mtaa wa Kimanga, eneo la ABC,  Mkuu wa kituo cha Polisi Tabata, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Bakari Goti aliwasihi wananchi kuharakisha michango ambayo itagharamia askari walioandaliwa vinginevyo alisema sheria iko wazi watakaokaidi kuchanga kwa kuwa wananchi wenyewe wameamua watapelekwa mahakama ya jiji wanakoweza kuhukumiwa kifungo na faini.

“Kitakachotokea ukishindw akulipa kwa miezi miwili ama mitatu sheria ndogo inasema wazi kwamba uongozi wa mtaa utatutaarifu na sisi tutakukamata na kukupeleka mahakama ya jiji ambako utahukumiwa moja kw amoja kwani haihitaji shaidi, na utahukumiwa”.

Hata hivyo alisem akutokana na ubinadamu watu ambao watakuwa na udhulu labda walikuwa wamelazwa katika kipindi hicho wanaweza kupewa muda, “Lakini nisingeshauri tufike huko.

Mkuu huyo wa kItuo aliwapongeza wananchi wa Kimanga kwa kuanzisha ulinzi wa namna hiyo na Alishauri mbali na kulinda usiku bado kuna haja ya kuwepo kwa doria za mchana kwani kumeanza kuripotiwa matukio ya watu kuvamia nyumba na kuiba mchana na hivyo kushauri wananchi kujenga tabia ya kuwatambua majirani na kubadilishana namba za simu ili iwapo kutakuw ana tukio la uharifu nyumbani kwako na kwa jirani iwe rahisi kupeana taarifa.

Nae Diwani wa Kinga ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kimanga, Manase Mjemaamewaonya wananchi wa Kata hiyo juu ya kuweka ngoma za usiku zijulikanazo kama Kigodoro katika sherehe na badala yake wametakiwa kufanya sherehe zao kwenye kumbi.

Akizungumza na wananchi juzi, wakati wa akuzinduliw akikundi cha Polisi Jamii, Diwani huyo amesema kuwa ngoma hiyo mbali na kuwa kero imekuwa ikisanbaisha watu kuibiwa na kuporwa mali zao kutokana na vijana wahuni kujiiingiza na kuvizia maeneo yaliyo karibu na ngoma hizo.

“Inasikitisha sana kuona kuwan awatu bado wanatoa vibali vy angoma hizi, hatutakubali watu wanakuwa wanaibiwa na kuporwa hivyo katika kata hii, kama mtu atakuwa na ngoma mwisho saa kumi na mbili ikiwa zaidi ya hapo wafanyiwe ukumbini ili wahuidhurie walioalikwa” alisema.

Mjema alisema kwa siku za karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kukatwa mapanga na kuporwa mali zao kutokana na ngoma hizo ambazo zimeshapigwa marufuku na kuhahidi kuwa kama ikitokea mkazi wa maeneo hayo atakaribisha ngoma hizo vifaa vitakavyotumika na yeye mwenyewe atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
 Wananchi wa Mtaa wa Kimanga jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkuu wa kituo cha Polisi Tabata, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Bakari Goti alipokuwa akifafanua umuhimu wa Ulinzi shirikishi juzi, katika mtaa huo, baada ya kukithiri kwa vitendo vya kiharifu hususan uporaji unaofanywa na Panya Road.
Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kimanga Manase Mjema akizungumza na wananchi wa eneo la ABC mtaani kwake juzi wakati wananchi hao walipoamua kuanzisha ulinzi wa Polisi Jamii baada yakuzidi kwa vitendo vya wizi wa kupora unaofanywa na vijana wajullikanao kama ‘Panya Road’ juzi.  Kushoto ni Mkuu wa kituo cha Polisi Tabata, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Bakari Goti.
Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kimanga Manase Mjema (kulia) akizungumza na Mkuu wa kituo cha Polisi Tabata, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Bakari Goti wakati wa mkutano wa wananchi katika eneo la ABC walioamua kuanzisha ulinzi kwa kutumia polisi jamii, ambapo wananchi hao watachanga pesa za kuwalipa vijana watakaofanya ulinzi.

No comments:

Post a Comment

Pages