Mabadiliko makubwa yanatarajiwa kufanyika ndani ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) baada ya semina elekezi kuhusu uendeshaji wa Baraza hilo kubwa la Waislamu nchini itakayofanyika kesho.
Semina hiyo elekezi itakayoshirikisha Masheikh wote wa mikoa,Makatibu wote wa mikoa na Wenyeviti wote wa Halmashauri Kuu wa mikoa inatarajiwa kutoa mwelekeo mpya wa jinsi chombo hicho kitakavyoongozwa.
Kwa mujibu wa Mufti wa Tanzania, ambaye kikatiba ya BAKWATA ndiye Sheikh Mkuu wa Baraza hilo, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, semina hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi jioni.
Akiongea na waandishi wa habari, Mufti Zubeir amesema BAKWATA imealika viongozi mbalimbali kutoka taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali.
“Tumewashirikisha viongozi wa TRA, Halal, Idara za Serikali na taasisi nyingine ili kutoa mada kadhaa zitakazosaidia Baraza letu kujitosheleza kiuongozi na kutoa huduma stahili na kamilifu kwa ajili ya kuiendeleza dini yetu, nchi yetu, watu wetun wadau nwetu na wenegine wote”, amesema Mufti na kusisistiza kuwa pamoja na kwamba semina hiyo iatakuwa ya kidini lakini itajikita zaidi kataika masuala ya uongozi wa kisayansi kuepuka baadhi ya makosa yaliyowahi kutendeka huko nyuma.
Amefahamisha kuwa masuala ya uongozi yatabeba nafasi kubwa kwenye semina hiyo elekezi yakiwemo pia ya mipango mahsusi ya Baraza, utiifu wa viongozi na uwajibikaji, changamoto na namna ya kuzikabili, utawala bora na maamuzi makini kwa faida ya Uislamu na nyanja nyingine.
Amesema baada ya mada hizo kutoka kwa viongozi wa taasisi hizo, semina itafunguliwa rasmi na yeye mwenyewe kuoanisha mada hizo zote na uongozo wa dini.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya BAKWATA yenye miaka 48 sasa kufanya semina elekezi ya mafunzo ya uongozi bora na utiifu kulingana na mabadiliko yanayotokea nchini na duniani kote.
Sheikh Abubakar ni Mufti wa tatu wa Tanzania tangu kuanzishwa kwake Desemba 23 mwaka 1968 chini ya sheria ya Bunge la Tanzania wakati wa Awamu ya Kwanza ya uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Weengine waliowahi kukalia kiti hicho ni Mufti, Sheikh Mkuu Hemed bin Jumaa bin Hemed na Mufti Sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba ambao wote wamekwishafariki.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir bin Ally (Kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Baraza Mkuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman Lolila (kulia kwake) na masheikh wengine.
No comments:
Post a Comment