May 17, 2016

BANK M KUENDELEA KUISAIDIA TAASISI YA BENJAMINI MKAPA KATIKA KUINUA SEKTA YA AFYA

 Mkurugenzi wa Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso akizungumza na waandushi wa habari jijini Dar es salaam leo kuhusu kuendelea kuisaidia taasisi ya Benjamini Mkapa ili kuinua sekta ya afya. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Dk. Ellen Senkoro. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Dk. Ellen Senkoro akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu ushirikiano wake na Serikali pamoja na sekta binafsi katika kufanikisha mpango wake endelevu wa miaka 5. Kulia ni Mkurugenzi wa Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso. 


NA GLORY CHACKY

TAASISI ya Benjamini Mkapa inatarajia kujenga vyumba vya upasuaji katika Halmashauri tatu za mkoa wa Simiyu ili kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Vyumba hivyo vinatarajia kujengwa katika halimashauri za Salala,Maswa na Busega lengo likiwa ni kusaidia afya ya mama na uzazi ambayo imeonekana kuwa tatizo hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salam,
 Mkurugenzi wa taasisi hiyo  Dk Ellen Senkoro alisema vyumba hivyo kila kimoja kinagharimu Milion 200 hadi kukamilika kwake.


“Tunampango wa kujenga thieta 15 katika halmashauri mbalimbali hadi sasa tunamejenga thieta tisa na zilizobaki tunamalizia kwa kipindi hiki kabla ya mwaka 2018” alisema Senkoro
Alisema katika kutekeleza mradi huo watashirikiana na sekta binafsi ikiwamo Benki M ambao wamekuwa wakiwasapoti kwa muda mrefu katika kuhakikisha wanafikia malengo la kuwaajiri wafanyakazi 1000.

Senkoro alisema kwasasa wamejenga nyumba 482 kwaajili ya madaktari na wauguzi ambapo hadio sasa wamekabidhi nyumba 310 na kusena wanatarajia kukabidhi vyumba vilivyobaki juni mwaka huu.

 Alisema lengo la taasisi hiyo ifikapo mwaka 2018 iwe imewafikia watu Bilioni 20 na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa benki M, Jacqueline Woiso alisema wataendelea kuwasapoti kwa hali na mali ili kuinua sekta ya afya kwani wafanyakazi wanahitaji vitu muhimu ili waweze kufanya kazi vijijini.

Benki hiyo inatoa Milioni 200 kila mwaka katika kusaidia shughuli za kijamii hasa vijijini.

No comments:

Post a Comment

Pages