May 13, 2016

KUTOKUCHEZA SOKA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA (TAIFA STARS) KUMENIKOSESHA NAMBA CHELSEA.

KAMA ningeweza kukutana Rais wa Shirikisho la Soka nchini ningemshauri namna bora ya kuanzisha vituo vya kukuza wachezaji chipukizi mikoa mbalimbali hapa nchini kwani hiyo ndio itakuwa njia sahihi ya kuinua soka la Tanzania ili kutoa fursa kwa wachezaji wa kitanzania kuweza kuchezea timu kubwa duniani.

Kwa sababu hakuna mamna ya kuweza kufanya ili tuweze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo ya mpira kwani bila kufanya hivyo kila siku tutakuwa tunapoteza muda ambao una thamani kubwa kama ungeweza kutumiwa vizuri.
Hayo sio maneno yangu bali ni ya  mlinda mlango wa kitanzania aliyewahi kufanya majaribio kwenye klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Abbas Pira “Barthez”wakati akizungumza na mwandishi wa makala hii ambapo anasema kwenye mafanikio ya soka hakuna njia za mkato lazima kuwepo kwa dhamira ya dhati ya kupewa msukumo jambo hilo.

Abas Pira ambaye aliwahi pia kuichezea timu ya Coastal Union miaka ya nyuma ilipokuwa ikishiriki Ligi Daraja la kwanza anasema ili Tanzania waweze kupata mafanikio lazima kuanza na vituo vya kukuza soka kama ilivyokuwa nchi nyengine duniani kwani hiyo ndio itakuwa dira na mabadiliko yatakayokuwa chachu ya kufikia ndoto za kuchukua kombe la dunia siku moja.

Anasema umuhimu wa vituo hivyo ndio utakuwa dira ya kulipeleka soka la Tanzania kwenye hatua kubwa kwa sababu wataweza kupata wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kuwa hazina kubwa kwa Taifa kwa kuzitumikia timu za Taifa kuliko ilivyokuwa sasa.
  “Unajua hata ukiangalia kwenye nchi za nje zinapata mafanikio makubwa kwenye soka kwa sababu ya kuwekeza kupitia timu za vijana na kufungua vituo vya soka hivyo jambo hilo kama likitiliwa mkazo hapa kwetu tutafika mbali “Anasema.

Aidha alisema ukiangalia kwa Tanzania vituo vingi vya kukuzia soka limejengwa kwenye baadhi ya mikoa michache na kuiacha mikoa yenye wachezaji wenye uwezo na vipaji kushindwa kupata fursa hiyo adhimu kwa ajili ya maendeleo yao.

Sambamba hilo lakini pia analitaka shirikisho hilo kuweka utaratibu mzuri wa kuunda kamati ya mawakala ambao watakuwa na kazi ya kuwachagua wachezaji ambao wanaweza kuwapeleka kwenye kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ikiwemo kuweka ufuatiliaji.

  “Unajua suala la kuundwa kamati ya mawakala ambao kila mwaka wanaweza kuwa na orodha ya wachezaji wangapi wamekwenda kufanya majaribio nje ya nchi na nafasi zao zipoje kwenye nchi ambazo wamekwenda kucheza “Anasema.
Pirra ni nani na alitokea wapi kabla ya kwenda Chelsea kwenye majaribio?

Abasi Pira anaanza kusema alianza kucheza mpira katika timu ya Mzambarauni mwaka 1994 iliyokuwa na maskani yake jijini Tanga baada ya hapo alionekana na Kocha Joseph Lazaro ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Mgambo Shooting  na kumpeleka timu ya Coastal Union ambapo alicheza mechi za timu hiyo wakiwemo Juma Mgunda,Mohamed Kampira,Saidi Mhando,Nyendi Mpangala ,Mwarami Saidi Deo Masanja na Sande Peter.

Hao ndio baadhi ya wachezaji ambao ninawakumbuka tulikuwa pamoja wakati nikicheza kwenye timu ya Coastal Union ambapo nilidumu kwenye timu hiyo mpaka mwaka 2005 wakati timu hiyo ilipokuwa ikishiriki Ligi daraja la kwanza.

Mlinda mlango huyo ambaye alisoma kwenye shule ya sekondari Popatlaly iliyopo Jijini Tanga kuanzia mwaka 2002 mpaka 2005 alianza kung’ara kwenye medani ya soka hapa nchinio baada ya kuwa mchezaji bora kwenye mashindano ya Umisseta.

Nini kilimpeleka nchini Uingereza?

Abasi anasema kuwa baada ya kumalizika kidato cha nne katika shule ya sekondari Popatlaly alipata nafasi ya masomo kusomea nchini Uingereza na hivyo kujikuta akilazimika kucheza mpira mtaani wakati anapokuwa ametoka shuleni .

Anasema alicheza mpira kwenye timu za mtaani kwa kipindi kirefu baadae watu walimuona na kumshauri kuongeza jitihada za kwenda kucheza kwenye timu kubwa na ndipo alipokwenda kufanya majaribio kwenye klabu za Chelsea kwenye dimba la Stanforde Brige na Klabu ya Birmingham City

Kwanini alishindwa kuchezea klabu ya Chelsea kama ilivyokuwa mipango yake?

Mlinda mlango huyo anasema kuwa licha ya kufanikiwa kucheza vema na kuvutia watu wengi kutokana na aina ya udakaji wake anapokuwa langoni lakini kilichomnyima nafasi ya kupata namba kwenye timu hiyo ni kutokana na kutouwa na rekodi ya kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania.

  “Kutokuwa na rekodi hii kumenifanya nishinde kupata namba ya kucheza Chelsea lakini pia kitendo cha nchi yetu ya Tanzania kushindwa kuwepo kwenye nafasi ya 70 B or kififa hilo ndio lilinikwaza kushindwa kupata kibali cha kucheza soka huko “Anasema.

Anasisitiza kuwa sababu kubwa ndio hivyo kwani hawajawahi kuichezea timu ya Taifa lakini pia kitendo cha Tanzania kutokuwepo kwenye renki za juu kwenye shirikisho la soka dunia ilikuwa ni kikwazo kikubwa cha yeye kufikia malengo yake.

  “Lakini pamoja na kupitia huku nimeenda pia kufanya majaribio kwenye vituo vya soka vya CV Academy ya North Ontony ya England na sasa nimerudi nyumbani Tanzania lakini pia nimesomea masuala ya Ukocha ngazi ya cheti kubwa zaidi nataka kuona kama ninaweza kupata nafasi ya kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.

Lakini kabla ya kufikia hatua ya kuchezea timu ya Taifa ya Tanzania hivi sasa anaangali namna yua kupata timu ambayo anawezea ili aweze kuonekana na baadae apata fursa ya kuitumikia timu hiyo kwani kwa sasa anafanya mazoezi kwenye timu za vijana za Boraska na Veteran kwa ajili ya kujiweka imara.
Nini malengo yake katika soka?

Pira anasema kwanza lengo lake kubwa ni kuhakikisha anapata namba ya kudumu kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ikiwemo kucheza kwenye timu yoyote hapa nchini ikiwemo Yanga,Simba na Azam FC ili kuweza kuonyesha uwezo wake aliokuwa nao.

Lakini pia anasema anaangalia namna ya kutafuta timu nje ya nchi ili kuweza kuendeleza kipaji chake kwani bila kucheza soka kinaweza kupotea na kutokuonekana kwake.

Anadhani watanzania wanakosea wapi kwenye soka?

Anasema kuwa Tanzania inashindwa kufanya vizuri kwenye medani ya soka kutokana na kutokuwepo kwa vituo vya kukuzia soka hasa maeneo ya mikoani kwani vingi vimekuwa vikijengwa mkoani Dar es Salaam wakati vipaji vingi vinatokea nje ya mkoa huo.

Sambamba na hilo pia akawageukia wachezaji wanaosajiliwa na vilabu na timu za Taifa za Tanzania kuhakikisha wanatimiza ndoto za wapenzi na mashabiki kwa kuvisaidia ili viweze kufikia malengo yake kwani kutokufanya hivyo watakuwa hawana msaada.

  “Lakini nisema pia aliyeweza kuliweka soka la Tanzania kwenye ramani ni Maxio Maxime ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa kwa sababu ujio wake hapa nchini uliweza kubadilisha mfumo wa soka na sasa tunahitaji kupambana zaidi “Anasema.

Historia ya mlinda mlango Pirra ambaye alizaliwa February 20 mwaka 1988 alianza kuichezea timu ya Coastal Union akiwa na miaka 10 ambapo rasmi ilikuwa ni mwaka 1998 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2005 kabla ya kwenda nchini Uingereza kimasomo.

Klabu ambazo aliwahi kuzifanyia majaribio ni Chelsea mwaka 2010, Birmingham City Football Club,Colchesterter United mwaka 2011 na mwaka 2012 alikwenda kufanya kujaribu pia bahati yake kwenye klabu ya MK Dons lakini pia aliwahi kuchezea klabu ya Legton Oriet FC.

Anataka kufikia wapi kisoka “

Pirra anasema kuwa malengo yake makubwa ni kuwa kama mlinda mlango Oliver Khan wa timu ya Ujerumani na Fabian Barthezi wa nchini Ufaransa aliyeisaidia timu ya nchi hiyo kuchukua Ubingwa mwaka 1998.

MAKALA HII  IMETAYARISHWA KWA HISANI YA TANGARAHABLOG

No comments:

Post a Comment

Pages