May 25, 2016

YANGA YATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO

Rais wa TFF, Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’. baada ya timu hiyo kuifunga Azam FC 3-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa. (Picha zote na Francis Dande)
Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akinyanyua juu Kombe baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akipiga mpira wa kichwa na kuifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Golikipa wa Azam akipishana na mpira uliopigwa na Amisi Tambwe.
Mashabiki wa Yanga.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi akiwa na wanayanga wakifurahia kombe mara baada ya kukabidhiwa . 
Wachezaji wa Yanga wakifurahia ubingwa mara baada ya kukabidhiwa Kombe la FA. 
Beki wa Azam, Aggrey Moris akimiliki mpira mbele ya Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva. 
Donald Ngoma wa Yanga akiruka juu kuwania mpira.
Mshambuliaji wa timu ya yanga Simon Msuva  akiwania mpira mbele ya beki wa timu ya Azam, 
Mchezaji watimu ya Yanga Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka kiungo watimu ya Azam Hamid Mao (kulia).
Kombe la ASFC.

No comments:

Post a Comment

Pages