June 02, 2016

Mwaka mmoja wa kampuni ya Shear Illusions

Kampuni ya Shear Illusions imehadhimsha mwaka mmoja tangu uzinduzi wa Kipodozi Pendwa cha LuvTouch Manjano. Kipodozi cha LuvTouch kilizinduliwa mnamo tarehe 31 May mwaka 2015 jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi aliyekuwa mke wa Waziri Mkuu wa zamani Mh. Mama Tunu Pinda katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Katika maadhimisho hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions mama Shekha Nasser amewashukuru wanawake  na Watanzania kwa ujumla kwa kufanikisha kutambulika kwa bidhaa za LuvTouch Manjano. LuvTouch ni Brand ya Kipodozi cha kwanza nchini inayomilikiwa na mwanamke mzalendo wa Kitanzania. Kupitia bidhaa hiyo pia imeanzisha Taasisi ijulikanayo kama 'Manjano Foundation' yenye lengo kuu ya kuwasaidia wanawake kiuchumi. Katika  mwaka mmoja tangu uzinduzi wa bidhaa za LuvTouch Manjano, Taasisi hiyo imefanikiwa kuwaelimisha zaidi ya wanawake 195 katika mikoa mitano nchini. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar, Arusha na Dodoma. 

Pia katika kipindi cha mwaka mmoja wameweza kuwakopesha wanawake mitaji ya vipodozi vya LuvTouch Manjano yenye thamani ya shilingi milioni 45 (TSh.45,000,000). Akieleza zaidi mama Shekha Nasser amesema ataendelea kuwashika mkono wanawake wenzake kadiri ya uwezo wake unavyoruhusu kwa lengo la kumkomboa mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa Ajira.Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wanawake walio washiriki wa mradi wa Manjano Dream-Makers na wadau (Mentors), washauri na watu waliojitolea kuwasaidia washiriki hao. 

Wanawake na washauri waliohudhuria hafla hiyo walimpongeza mama Shekha Nasser kwa moyo wake wa kujitolea na kuwabeba wanawake vijana. Mmoja wa wazungumzaji na mdau wa mradi, mwanasaikolojia maarufu aunt Sadaka Gandi alisema, ameishi na wanawake wengi nchini lakini hajawahi kuona Mwanamke mwenye moyo wa kujitolea kama wa Shekha. Amewaasa wanawake walionufaika na mradi huo kufanya kazi kwa bidii kupitia Mradi huo kwa kuwa wao wanabahati sana kunufaika kwa kuwa wapo wanawake wengi nchini wasiokua na kazi na wangetamani kunufaika lakini wamekosa nafasi hiyo

No comments:

Post a Comment

Pages