Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba
mjini Nkansi akiwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa, Agosti 23, 2016. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu
yeyote atakayekutwa na hatia ya kuvunja sheria kwa kuvamia na kuharibu
mazingira ya msitu wa Mfili ambao ndiyo chanzo pekee cha maji cha Wilayani Nkasi
atatozwa faini ya sh. milioni 70 pamoja na kifungo miaka saba jela.
Katika
kuhakikisha hatua zinachukuliwa Waziri Mkuu amemkabidhi mkuu wa wilaya ya
Nkasi, Said Mtanda kitabu cha sheria kitachomuangoza katika kuwachukulia hatua
wale wote watakaobainika kufanya uharibifu katika chanzo hicho cha maji.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni
(Jumanne, Agosti 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa mji Mdogo wa Namanyere
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanya vya Sabasaba.
“Mkuu
wa wilaya akishindwa kuwachukulia hatua za kuwaondoa wananchi na kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu na
kuanzisha makazi au kufanya shughuli za kijamii naye atakuwa jipu,” alisema.
Waziri
Mkuu alisisitiza kuwa maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto ya
upatikanaji wa maji baada ya wananchi kuvamia katika vyanzo vya maji na kufanya
shughuli za kibinadamu hivyo kusababisha vyanzo vingi kukakuka
“Serikali
haitakubali kuona mtu anaharibu chanzo cha maji. Wananchi mnatakiwa kuwa
walinzi wa maeneo hayo na atakayekutwa anachunga mifugo, analima, kukata nyasi
au kufanya shughuli zozote za kijamii ndani ya maeneo hayo atachukuliwa hatua
kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Awali
Waziri Mkuu alikagua mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfili ambalo mwanzo
lilikuwa na ujazo wa lita 1,500 ambapo litakapokamilika litakuwa na ujazo wa
lija 248,067 hivyo kuwezesha wakazi 82,689 kunufaika.
Akizungumza
kwenye eneo la mradi mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili, Mkurugenzi Mtendaji wa
wilaya ya Nkasi, Julius Kaondo alisema hadi kukamilika mradi huo unatarajiwa
kugharimu sh trilioni 1.011 ambapo Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetoa sh.
milioni 500 na OOfisi ya Rais TAMISEMI itatoa sh. milioni 500.
Mkurugenzi
huyo alisema mradi unakabiliwa na changamoto ya ukosefu umeme ppamoja na mitambo ya kusukuma maji kwa
kutumia nishati ya umeme, ambapo aliiomba Serikali kuipatia halmashauri hiyo
sh. milioni 222.576 ikiwa ni gharama za kupeleka umeme kwenye eneo la mradi na
kununua mitambo.
Mbali
na kutembelea mradi wa upanuzi wa bwawa, pia Waziri Mkuu alitembelea hospitali teule
ya wilaya ya Nkasi na kuzindua wodi mpya yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 72 kwa
wakati mmoja.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 24, 2016.
No comments:
Post a Comment