Mhamasishaji Mkuu wa Siasa za Chadema kwa njia ya nyimbo na sanaa Fulgency Mapunda akizungumza na waandishi wa habari huku akibubuji kwa na machozi
Mhamasishaji Mkuu wa Siasa za Chadema kwa njia ya nyimbo na sanaa Fulgency Mapunda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Agosti 21 kuhusu hatma yake ndani ya chama hicho.
NA MWANDISHI WETU
Mhamasishaji Mkuu wa Siasa za Chadema kwa njia ya nyimbo na
sanaa Fulgency Mapunda amewataka viongozi
wa wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Chadema) kumfahamisha hatima yake ndani ya
chama hicho akiwa kama mhamasishaji mkuu wa Program za Chama kupitia siasa.
Aidha anawata viongozi hao wamfahamishe hatima ya Idara ya
Sanaa ndani ya Chadema kama kitengo
mahususi cha kuhamasisha Program za Chama kupitia sanaa.
Akizungumza na
waandishi wahabari jijini Dar es Salaam jana
Mapunda alisema amefikia hatua hiyo
baada ya kutokea sintofahamu kati yake
na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent
Mashindi.
Mapunda alisema tangu Mei mwaka huu imetokea sintofahamu
kati yake na Dk.Mashindi kwa kufanya
mageuzi ya kimfumo ndani ya Chadema.
“Figisufigisu hizi zinafanywa na wakurugenzi wanaomzunguka
Katibu huyo,akiwemo John Mrema na Reginald Munishi dhidi yangu,”alisema
Mapunda.
Mapunda alisema pamoja na umuhimu wa pekee wa Idara ya Sanaa
katika kuhamasisha program za Chadema katika kutengeneza taswira chanya ya
Chadema mbele ya macho ya umma,bado idara hiyo imefutwa na Katibu Dk. Mashindi.
“Swali langu kwa bwana Mrema na Munisi mbona mchujo huu
haujawagusa kwa wale wenye mrengo wa kwao na walitumia vigezo gani kwa sababu
karibu wote wamerudishwa na kuniacha mimi mwenye sifa ,taaluma na uzoefu
,”alihoji Mapunda.
Mapunda alimtaka Mwenyekiti wa Chadema Taifa,na kamati kuu
watambue mchango wake na kujua hatima yake ndani ya Chadema.
“Nataka nijue iwapo wamenitelekeza pamoja na ukweli kwamba
tulikua pamoja siku zote za mapambano kwa miaka zaidi ya 15,tukipambana katika
dhiki na raha,” alisema Mapunda.
Baadhi ya nyimbo alizotunga na kuimba kama mhamasishaji Mkuu
wa Chadema ni Chadema Chadema Peoples
Power, Tuyamwage Mafisadi , Operesheni Sangara, Wabunge wa Chadema
Twende, Fagia uwanja utakate MBoe apite, Chadema Mwendo mdundo.
Nyingine ni Chadema tuko tayari,vua gamba vaa gwanda, kwa
heri mafisadi, haturudi nyuma, chagua shangilia, chadema ni dara na Dikteta
uchwara.
No comments:
Post a Comment