Watoto na wananchi wa kijiji cha Majichumvi
wilayani Mvomero wakionyesha mabango wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa
aliposimama kijijini kwao kuwasikiliza Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Stendi mpya ya mabasi la
Msamvu mjini Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.
Pia aliwataka wafugaji hao kushirikiana na Serikali
katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji
na majosho ili ufugaji wao uwe na tija.
Waziri Mkuu
ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea kiwanda
cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Movomero.
Hata hivyo Waziri
Mkuu alisema kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi kitawezesha mifugo
yao kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa ya kutembeza mifugo umbali
mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija ndogo.
Akizungumzia
kuhusu uwepo wa kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri Mkuu
alisema kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa
wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo.
“Uwepo wa
viwanda katika maeneo yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo katika
maeneo yetu ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Viwanda
ndiyo vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati,” alisema.
Kwa upande
wake Mkurugenzi na Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu
alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo
1,500 kwa siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi
huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje ya
nchi hasa Uarabuni kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa
na mvuto maalum katika nchi hizo.
“Mbali na
uwekezaji huu wa kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika mnyororo wa
thamani kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi kuzalisha viatu,
mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje
ya nchi,” alisema.
Mrutu
alisema nia yao ni kuitikia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka viwanda
vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga
kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa hizo.
Aliongeza
kuwa uwepo wa kiwanda hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza majani,
mifugo na mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari wameanza
kuhamasisha jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero, Ngerengere na sehemu
zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa hiyo.
Katika
hatua nyingine
Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero kufanya mapitio ya mashamba
ili kujua wamiliki wake na kama hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka wa
kuyatwaa na kuyarudisha mikononi mwa Serikali.
Waziri Mkuu
alitoa agizo hilo wakati akijibu ujumbe uliokuwa katika mabango yaliyobebwa na
wananchi wa kijiji cha Maji ya Chumvi wilayani Mvomero waliosimamisha msafara
wakati ukitokea kwenye kiwanda cha nyama.
OFISI YA
WAZIRI MKUU,
JUMANNE,
AGOSTI 02, 2016
No comments:
Post a Comment